LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

SOLOMONI MUKUBWA ASIMULIA KILICHOSABABISHA KUKATWA MKONO


Jina la Solomoni Mkubwa muimbaji wa muziki wa Injili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) limekuwa gumzo kila pembe ya nchi ya Tanzania kutokana na wimbo wake wa Mfalme wa amani ambao kwa asilimia kubwa umeonekana kuwagusa watu wengi wakristo na wasio wakristo.
Mwimbaji huyo ambaye ni mlemavu wa mkono wa kushoto, kwa sasa masikani yake yapo jiji la Nairobi nchini Kenya alisema kuwa, wimbo wa Mfalme wa amani aliutunga ili kumtukuza Mungu baada ya kumuepusha na kifo ambacho kingempata baada ya mama yake wa kambo kumroga na kusababisha mkono wake kuvimba na alitibiwa na madaktari bingwa bila mafanikio na alipoenda kwa waganga wa kienyeji hakupona.
“Nikiwa na miaka 12, nilipata matatizo ya uvimbe wa mkono wangu wa kushoto ambao uliweka uvimbe wa ajabu na hakuna aliyefahamu chanzo kilikuwa nini, kimbe ni mama yangu wa kambo ambaye alikuwa mchawi mkubwa na mwenye wivu ndiyo maana aliamua kunidhuru kwa nia ya kuniua.
“Niliugua kwa muda wa miaka mitatu, wazazi wangu walihangaika kunipeleka kwa wataalam wa hospitali mbalimbali na kisha kwa wanganga wa kienyeji bila mafanikio, na baada ya muda huo kupita ilianzishwa hospitali moja na wazungu karibu na nyumbani kwetu, na nilipopelekwa hapo wataalam hao nao walishindwa na kushauri nikatwe mkono wangu kwa lengo la kunusuru uhai wangu.
“Hivyo ndivyo nilivyopoteza mkono wangu na kubaki nao mmoja kutokana na chuki ya mama yangu huyo, lakini ahimidiwe Mungu wa Ibrahimu kwa kuwaongoza wataalam hao kugundua njia hiyo, japo nilifika na kwa waganga wa kienyeji nao wakawa hawanauwezo wa kuniponya,” alisema Solomoni.
Mwimbaji huyo ambaye mwaka 2009 utabaki kuwa kumbukumbu maishani mwake kutokana na kupata kibali cha hali ya juu nchini Tanzania alisema kuwa, kutokana na maisha hayo ndiyo maana aliamua kutunga wimbo wa Mfalme wa amani kwa lengo la kumtukuza Mungu kwa matendo makuu aliyomfanyia.
“Wimbo wangu wa Mfalme wa amani niliamua kuuimba baada kuvuka katika shida hizo na albamu yangu kuipa jina la Mungu mwenye nguvu, na kuna maneno niliweka kwenye kibao hicho kwamba; ukiwa na shida usiende kwa waganga wa dunia, mwite mfalme wa amani, yeye anajibu maombi.
“Baada ya kupona mkono wangu, mama yangu wa kambo alikiri kunifanyia kitendo hicho, lakini mimi nilipookoka nilimsamehe, kwa muda mfupi naye aliokoka kutokana na pigo kali alilopata mwanaye kwa kuumia jicho alipokuwa anachezea chelewa kwenye moto ambalo liliruka na kuharibu babisa jicho lake.
Akielezea sababu za yeye kuhamia Kenya na kuondoka kwao Kongo, Mukubwa alisema kuwa, alioneshwa na Mungu aende kuishi huku na kiroho alilelewa kwa ukaribu na marehemu Angela Chibalonza aliyeonekana kama mama yake mzazi na alikuwa mshauri wake wa karibu katika huduma.
Akielezea vikwazo alivyokumbana navyo kabla ya kuvuma Tanzania, Mukubwa alisema kuwa, kabla ya hapo alikuwa anavujwa moyo na kwa kubezwa na baadhi ya watu kwa kumuona msanii mchanga asiye na kitu katika fani ya muziki wa Injili.
Mwimbaji huyo tayari ana albamu mbili ya kwanza ilijulikana kama Sijaona rafiki na ya pili, Mungu mwenye nguvu ambayo ndiyo imemtambulisha katika anga ya muziki wa Injili.


Newer Post Older Post

One Response to “SOLOMONI MUKUBWA ASIMULIA KILICHOSABABISHA KUKATWA MKONO”

Anonymous said...

JAMANI KWELI MUNGU NI MKUBWA BASI AZIDI KUMPA MAFANIKIO HUYO KAKA ZAIDI YA HAPO NA ASIKUBALI HATA SIKU MOJA BINADAMU AKAMKATISHA TAMAA KWANI HAKUNA MWENYE UWEZO WA JAMBO LOLOTE HAPA DUNIANI ZAIDI YA MUNGU. Kila ka Kheri Kaka Solomoni Mukubwa. KAZI ZAKO NI NZURI SANA.
Mama Mario tbt Kisukuru