Alex Msama: SIMWACHI ROSE
Msama alifikia hatua hiyo ikiwa ni saa chache toka kuingia mtandao kwa habari hii iliyoandika kuwa; ROSE MUHANDO AIPASUA NDOA YA MTU.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa, toka habari hiyo isomeke kwa wadau wengi, amekuwa akipigiwa simu za kumpa pole kwa tukio hilo .(Msama kushoto akifafanua jambo ndani ya ofisi ya TGM)
“Hii habari imenipa wakati mgumu sana , kila mtu pole, pole, mpaka nimekatisha usingizi leo. Mmi sikubali, nataka kujua aliyewaletea nyinyi hizi habari. Unajua hata Meneja wa Rose (Muhando), Nathan naye amenipigia, kaniuliza nani anayeleta habari mtandaoni?” Alisema Msama.
“Mimi na Rose tuko karibu sana , lakini kikazi na siwezi kumwacha, nimetoka naye mbali. Nimefanya naye matamasha mengi mengi, hata hivi karibuni tutafanya jingine la Pasaka,” alisema Msama.
Aliongeza kuwa, kama kuna wanaofikiria vibaya kuhusu ukaribu wake na Rose, “basi wanakosea sana, ni kwa ajili ya kazi tu na kwa hilo mimi siwezi kumwacha Rose kwa sababu hatuna kitu kingine kibaya baina yetu na tunaheshimiana sana,” alisema Msama.
Akipangua zaidi ishu hiyo, Msama alisema kuwa, yeye, mkewe, Rose na meneja wa Rose, Nathan wanamtafuta ‘mchawi’ anayewawangia usiku na mchana na kusababisha pole zisizokuwa na sababu.
One Response to “Alex Msama: SIMWACHI ROSE”
Umaarufu jalala. Hata iweje watu wataendelea kusema na kuzusha mambo na huo ndio ukweli wenyewe wa maisha hapa duniani. Hata ukifa napo utasemwa tu! Walimsema na kumzushia mambo Yesu Kristo sembuse Rose Muhando?
Ni vizuri kukanusha lakini wakati mwingine ni vizuri pia kuyaacha mambo hayo yakajifia yenyewe. Cha muhimu ni kumtegemea Mungu na kujikabidhi kwa Mungu kwa nia ya kweli. Mengine yote ni madogo.
Poleni sana kwa changamoto hii. Mungu Awe nanyi daima!
Post a Comment