LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

Raymond Jackson: Ukimwi hautupati tukifuata Biblia


KUKUA kwa muziki wa Injili leo hii, sio jambo geni tena kutokana na wimbi kubwa la wadau wa fani hiyo kuongezeka kila kukicha, huku vijana wakiwa wengi kwenye jamii inayofanya kazi hiyo. Raymond Jackson ni muimbaji wa njimbo za Injili ambaye ameanza rasmi kazi hii tangu mwaka 2006, ambapo tangu wakati huo hadi sasa amekuwa ni moja ya watumishi wanaofanya vema kwenye fani hiyo.
Akizungumza na Championi Ijumaa, mwimbaji huyo anayejulikana pia kwa jina la Ray, anasema kwamba jambo kubwa lililomfanya kuamua kufanya muziki huo si kwa matakwa yake bali ni wito uliokuwamo kwa muda mrefu ndani ya moyo wake.
Kutokana na sababu hiyo, aliamua kufanya jukumu hilo alilopewa na Muumba kwa moyo wote, kwa imani kuwa siku zote kazi ya Mungu hufanyika kwa kujituma kwa moyo na si vinginevyo. Aidha Ray, anasema kuwa suala la kufanya muziki wa Injili linategemea pia kulelewa na kukuzwa kiroho ambapo kwa sasa anaabudu katika Kanisa la Maximum Deliverance lililopo chini ya Mchungaji John Simon. Sambamba na uimbaji kwa lakini anafanya kazi katika kwenye Kampuni ya FM Wasambazaji.
 Kadhalika muimbaji huyo anaeleza kwamba, tangu ajikite katika ulimwengu wa nyimbo za Injili, yapo baadhi ya mambo anayoamini kuwa hayapo sawasawa hasa kwa waimbaji wenyewe.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na  miongoni mwao kutumia neno la Mungu kwa ajili ya  kupata umaarufu mbele ya jamii, pia  ushirikiano mdogo kwa baadhi ya waimbaji waliotoka na wale ambao wanachipukia, jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa na chipukizi wengi.
“Waimbaji waliotangulia katika kazi hii ya kumsifu Mungu watambue kwamba ni Mungu pekee ndiye aliyewainua, kwa hiyo waache kuwavunja moyo chipukizi, wakumbuke kwamba hapo walipo ni kwa msaada  na neema za Mungu tu na si kwa ajili ya nguvu zao,” anasema Ray na kuongeza kuwa.
“Unakuta chipukizi anaomba kumshirikisha muimbaji mwenye jina lakini kwa kuwa hawatambui kwamba kazi hii ni ya Mungu wanakataa, ningependa watambue kwamba hakuna muimbaji wa Injili mchanga bali ni kwamba wote tuko kwenye foleni, wao wametangulia na wengine watafuatia.”
Mbali na hayo anasema anafurahishwa na baadhi ya waimbaji ambao hawana dharau na wenye ukarimu kwa waimbaji wanaochipukia na wanajua kwamba kazi ya uimbaji siyo kwa ajili ya maslahi binafsi, inalenga hasa kumsifu Mungu na kuponya roho za wanadamu.
Ray ambaye pia ni mtoto wa tatu kuzaliwa katika familia ya Mzee Jackson anaongeza kuwa kutokana na kuzidi kusambaa kwa maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, ameamua kuwa mstari wa mbele katika kupinga vita ya kuenea kwa ugionjwa huo.
“Naamini Biblia takatifu ndiyo mambo yote, kwa sababu hiyo kama tukifuata maandiko hayo ni wazi kuwa suala la kufanya zinaa litakuwa ndoto kwa maana kwenye kitabu hicho Mungu ameweka kila kitu bayana bila kificho.
 “Shetani anatumia mbinu nyingi, jamii isipolitambua hili tunaweza kujikuta tunaangamia, hakuna jingine katika kujikomboa na hali hiyo kwa kumkimbilia Yesu, kwa jina lake hakishindikani kitu,” anasema Ray.
Upande wa albamu yake anasema amekamilisha nyimbo 10 na itajulikana kwa jina la Nipige Picha Leo, ambapo kati ya hizo kuna Uzuri Wako ambao ndiyo umemtambulisha na kumpa umaarufu.
Nyimbo nyingine ni Nakushukuru Mungu, Kilio Chako, Upendo, Moyo Wangu Tulia, Mke Si Nguo, Nipige Picha Leo, Bora Subiri na nyinginezo.

Newer Post Older Post