JIHADHARINI NA MANABII WA UONGO
Ndugu zangu katika Bwana Yesu Kristo, nawaomba wote muwe makini kipindi hiki ambapo tayari Manabii wa uongo tayari wamesingia na wanafanya kazi kama watumishi wa Mungu wa kweli. Hawa utawajuaje, huwezi kuwatambua kwa kuwatazama kwa macho ukawatambua, lakini utawatambua kwa matendo yao.
Yesu alilionya kanisa lake kuhusu makristo wa uwongo. Imo katika Biblia, Mathayo 7:15, 21-23 "Jihadharini na manabii wa uongo watu wanowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa wa mwitu wakali. 21-23, Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu." Yesu alilionya kanisa lake kuwa kitambo kidogo kabla ya kuja kwake mara ya pili yule anayempinga Kristo atajaribu kufanana naye Yesu hasa kuwaambia watu kuwa yesu amerudu mara ya pili Imeandikwa Mathayo 24:4, 5, 24-26 "Yesu akajibu, akawaambia angalieni mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. 24-26 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi wakiwaambia yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki." 2 Wathesalonike 2:3 - 4 "Mtu awayeyote asiwadangaye kwa njia yo yote maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu, ama kuabudiwa hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu."
2 Wathesalonike 2:8-10 "Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambapo Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake; yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake shetani kwa uwezo wote na ishara na ajabu za uongo na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanao potea kwa sababu hakuipenda ile kweli wapate kuokolewa."
Post a Comment