LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

ASKOFU AISHI NA WAKE WAWILI

 Ni dhahiri sasa kuwa dunia inaelekea ukingoni, matukio yaliyotabiriwa na manabii wa kale yanazidi kutimia, na mfano hai ni Askofu Mkuu wa huduma iliyojitwalia umarufu mkubwa ndani ya mkoa mmoja mashuhuri nchini ambaye anakabiliwa na skendo ya kuishi na wanawake wawili.
Habari za uhakika zimepenya ndani ya mtandao huu  zinasema kuwa, askofu huyo ambaye siku za nyuma alifanikiwa kujikusanyia kondoo wengi kutokana na huduma yake, anadaiwa kumuweka kinyumbaa katibu muhtasi wake ambaye ni mke wa muumini wake.
Mpenyesha habari wetu aliendelea kudokeza kuwa, siku moja askofu huyo aliibuka katika huduma yake na kutangaza kuwa Bwana amemuonesha mwanamke anayeishi naye si mkewe bali ubavu wake ni mke wa muumini wake ambaye alipaswa kumuoa.

Alisema, baada ya kutolewa kwa kauli hiyo na Mtumishi huyo wa Mungu, baadhi ya waumini waliinamisha vichwa vyao chini huku kila mmoja akisema lake, na wengine kuamua kujiengua kwa madai kuwa wanakopelekwa siko.
“Mimi nilikuwa muumini wake, nilishuhudia askofu akitamka uchafu huo mbele ya madhabahu ya Mungu, hakika moyo wangu uliumia kiasi kwamba nikakosa amani ya kuendelea kuabudu mahali hapo,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Anayoyafanya Mtumishi huyo ni abu. Ukiacha suala la kumuweka kinyumba muumini huyo, kuna wanawake wengi sana amewaangusha katika dhambi ya uzinzi na baadhi yao ndoa zao zimevunjika kwa sababu walikuwa wepesi wa kukubali kufanya mapenzi na askofu huyo.”
Mtoa habari wetu ambaye baada ya kujinasua kwenye kanisa hilo, naye aliamua kuanzisha huduma yake, aliendelea kusema: “Hakuna mwanamke mrembo aliyeabudu kanisani hapo asimwangushe katika dhambi ya uzinzi. Wengi wao amekuwa akizini nao kwa mgongo wa kwenda kuwaombea kwenye chumba maalum.”
Baada ya kupenyezewa habari hizo, gazeti hili lilimwendea hewani mke halisi wa Mtumishi huyo ambaye alikanusha madai ya mumewe kuwa na nyumba ndogo.
Hata hivyo, Mtumishi huyo ambaye kwa sasa amehamishia huduma yake jijini Dar, hakauweza kupatikana kwa sababu yupo nje ya nchi.

Pamoja na hivyo, mtandao huu ulifanikiwa kuzungumza na baadhi ya watumishi wa Mungu ambao walielezea mitazamo yao juu ya mtumishi huyo wa Mungu ambaye mara nyingi hujiita Nabii.
Askofu Nicholas Suguye wa Huduma ya Neno la Upatanisho iliyopo Bustani ya Edeni Kitunda Kivule, Dar es Salaam alisema kuwa yeye binafsi anakerwa na na kitendo cha mtumishi mwenzao kufanya hivyo, kwani hata waumini anaowaongoza ameshawaambukiza roho hiyo ndiyo maana wamekuwa wepesi kuanguka nao kwenye dhambi ya uzinzi. 
Suguye, aliwataka Watanzania kujihadhari na manabii wa uongo wanaovaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali kwa sababu mti  mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 
“Kipindi hiki Watanzania wanatakiwa kuwa makini kwani manabii wa uongo tayari wapo. Biblia inasema kuwa, kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa katwa na kutupwa motoni na watatambuliwa kwa matunda yao.''
“Si kila mtu anayesema, `Bwana, Bwana,' ataingia katika Ufalme wa mbinguni, ila ni wale wanaofanya mapenzi ya Baba  na siku ile itakapofika wengi watamwambia: Bwana, Bwana, hatukutoa unabii na kufukuza pepo kwa jina lako,” alisema Suguye.
Kwa upande wa Mchungaji Christophila Kalata wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), aliliambia Risasi Jumamosi kuwa anatambua kila kitu kuhusu Mtumishi huyo na skendo yake ya kuishi na wake wawili.
“Namtambua huyo Mtumishi, najua kwamba anaishi na wake wawili, pia yapo mengi. Kimsingi ni kwamba hafai kuitwa Askofu na ni vema huduma mpya ikaingia kwenye Kanisa lake ili kuwaokoa kondoo wanaoangamia kupitia mgongo wake,” alisema Christophila.

Newer Post Older Post