LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

COSMAS CHIDUMULE: INJILI IMEGEUZWA BIASHARA

Namshukuru Mungu kwa kutuamsha wazima tena siku ya leo, niwape pole wale wote wanaosumbuliwa na changamoto ya afya zao.
Kila kukicha makanisa yamekuwa yakiota kama uyoga mengi yakiwa na majina ya kigeni. Mimi sipingani na kuibuka kwa makanisa hayo kwani natambua wazi kuwa kusudi kubwa la kuanzishwa ni kuhubiri neno la Mungu ili watu walioanguka katika dimbwi la dhambi wamrudie Mola.
Endapo kusudi hilo lingekuwa linafanywa kama agizo la Mungu linavyosema “enendeni mkafanye mataifa yote kuwa wanafunzi…na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru”. Viongozi wa makanisa hayo kama kweli wangekuwa na moyo wa dhati kuihubiri kweli ya Mungu, leo hii nchi yetu isingekuwa na waumini wanaovaa ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu.
Kila siku ya Jumapili nyumba za ibada huwa zinajaa watu ambo ukifika kanisani na kuwaona kwa macho, hakika utasema hata leo ikiwa kihama wao moja kwa moja wataingia mbinguni. Viongozi wao ndiyo zaidi hasa ukiwaona wakiwa wamevaa mavazi yao ya kitumishi pamoja na kuongea maneno ya unyenyekevu hakika utasema kama ni utakatifu basi ni huu.
Lakini wanavyoonekana kwa macho sivyo walivyo mioyoni mwao. Waumini siwezi kuwalaumi kwa sababu baadhi yao huenda kanisani kama desturi lakini suala la kuondoka wakiwa wamebadilika kitambia hilo huwa halina nafasi. Mbaya zaidi injili ya siku hizi imekuwa ni ya kuhubiri mafanikio badala ya kukemea watu wasifanye dhambi.
Kutokana hali hiyo kunisumbua kwa muda mrefu akilini mwangu, nililazimika kumtafuta mchungaji na mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Cosmasi Chidumule ili kuliweka sawa jambo hili. Mara baada ya kufanikiwa kumpata, nilimtupia swali la kwanini injili ya leo imejaa maombi ya watu kufanikiwa badala ya kukemea maovu ili waishi maisha ya utakatifu na baraka zikawafuata?.
Chidumule hakupenda kupindisha maneno bali alisema wazi kuwa injili ya miaka ya hivi karibuni imegeuka kuwa biashara badala ya kuhubiri kweli ya Mungu. “Baadhi ya watumishi wa Mungu wamegundua kwamba, watu wengi wanaishi maisha ya shida na wanauhitaji wa mafanikio ya harakaharaka, hivyo ili uwapate wengi ni vema wakagusa eneo hilo kwa kutambua kuwa watamiminika kanisani na kuwahubiri injili ya mafanikio huku wao wakiwaahidi kutoa vitu flani ili wafanikiwe zaidi,” alisema Chidumule.
Chidumule aliendelea kusema kuwa, ili kudhihirisha watumishi wengi wa Mungu wamegeuza injili kuwa biashara, kila kukicha utasikia matangazo yanayoelezea kupokea baraka huku wakiwashinikiza kwa kutumia baadhi ya maandiko kuwa wasipotoa vitu kadhaa maisha yao yatakuwa ya dhiki mpaka mwisho wa maisha yao.
Kitu kingine ambacho kimekua kikinishangaza ni kuona watumishi wa Mungu kuhubiri injili ya kupaka mafuta kwa kuogopa kuwapoteza waumini wenye ‘shekeli’ambao huonekana msaada mkubwa kanisani hapo. Ni jambo la kawaida kwa waumini wanaufundishwa kweli ya Mungu kuwa wala rushwa, matapeli, watukanaji, wasengenyaji wanaouza dawa za kulevya na wakwepaji wakubwa wa ushuru kwa wafanya biashara.
Kitu cha kujiuliza ni kwamba, watumishi kama hawa, wataenda mbingu ipo siku Mungu akiwaita? Je, waumini wao nao wanao onekana kuwa watakatifu siku ya ibada na wakitoka nje ya hapo wanakuwa sawa na watu wasiomujua Mungu, nao siku ya mwisho watakuwa upande gani? Mimi na wewe hatuwezi kuwahukumi, isipokua anayejua hatima yao ni Mungu peke yake.
Katika mazungumzo yangu na Chidumule nilimuuliza kwanini amekuwa kimya katika anga ya muziki wa Injili? Muimbaji huyo aliyetesa na kibao cha Yesu ni Bwana mwaka 1998 alisema kuwa, baada ya kutoa albamu ya Yesu ni Bwana mwaka huo na 2001 kutoka na santuli ya Kimbilia kwa Yesu, aliondoka nchini Marekani kwa ajili ya kuhubiri kwa njia ya uimbaji na uinjilisti hiyo ikiwa ni mwaka 2006.
Mwaka 2007 alirejea nchini na kwenda kupata elimu ya masomo ya dini katika Chuo cha Utumishi Efatha na alipomaliza mwaka 2008 alifanya mazoezi ya kichungaji katika kanisa la Efetha. Mwaka 2009 alitumwa na kanisa hilo kwenda kujenga kanisa Songea. Kitendo hicho kilimfanya ashindwe kuvuma tena katika fani ya muziki wa Injili.

Picha kwa hisani ya www.strictlygospel.wordpress.com



Newer Post Older Post