JANE MISSO AKUMBWA NA SKENDO
Mtandao huu kwa masikitiko yaliyoambatana na maswali ya siamini jamaa mmoja anajihusisha na biashara za kuuza spea za magari aliyejitambulisha kwa jina la Benson Mafuwe alisema kuwa mwanzoni mwa mwezi wa tisa mwaka 2007 alikutana na muimbaji huyo na kumuomba amsaidie kukamilisha albam yake iliyotambulika kwa jina la ‘0M0Y0’ ambapo bila ya kuweka kinyongo na mimi mwenyewe ni mmoja wa watu waliokoka nikakubali kumsaidia lakini kilichokuja kutokea siamini mpaka hivi sasa naongea na wewe.
‘Unajua nasema siamini kwasababu gani sikutegemea mtu kama Jane angekuwa tapeli kiasi hiki’ alidai Benson
Akiendelea kusimulia Benson alisema kuwa baada ya makubaliano yao kufikia hatua nzuri waliongoza hadi kwa Mwanasheria wake aliyemtaja kwa jina moja Rwiza wa kampuni ya Azania Law Chambers na kuandikishiana mkataba na kumkabidhi fedha taslimu shilingi milioni kumi ‘10,000,000’ zitakazotumika kutengeneza Audio na Video Cd za albam hiyo maandalizi ya uzinduzi pamoja kuwalipa vikundi mbalimbali vitavyoalikwa siku ya uzinduzi na kukubaliana chochote kitakachopatikana kwenye albam hiyo ya ‘OMOYO’ basi wagawane pasu kwa pasu, mkataba ambao uliingiwa September 17, 2007 na Ijumaa kubahatika kupata nakala ya mkataba huo.
‘Kiukweli tangu niingie naye mkataba hakuweza kunishilikisha kwa chochote kile hadi siku alipozindua albam yake na kushuhudia akipata fedha taslimu milioni nane kwani mgeni rasmi alitoa milioni tano na watu wengine walichanga kiasi cha milioni tatu kwa ajili ya harambee iliyopitishwa ukumbini hapo naye hakuweza kunipa taarifa zozote zile baada ya muda nikimpigia simu anakuwa hapokei nikibadili namba akipokea ananiambia yuko Nairobi nimsubiri harudi aje aniludishie fedha zangu kitu ambacho ajatekeleza hadi leo hii’ alidai Benson.
Katika kuendelezea kusimulia Benson hakuishia hapo alisema kuwa amefanya jitihada nyingi sana za kutaka angalau aludishiwe kiasi cha fedha zake alizozitoa lakini imeshindikana kilichobaki suala hili kulifikisha Mahakamani.
‘Mi naona Mahakama ndio itakayoamua hatima ya suala langu kwani nimevumilia zaidi ya miaka mitano bali ya kupata ufumbuzi wowote’
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo gazeti hili liliwasiliana na Jane Miso ambapo baada ya muandishi kujitambulisha na kisha kumsomea mashtaka yake alidai kuwa yuko kwenye basi akielekea Kahama kwa hiyo si vizuri kuzungumzia suala hilo akiwa safarini.
‘Ngoja nifike nitakupigia tuongee vizuri’ alisema Jane.
Baada ya kama dakika tano Jane alipiga simu na kuuliza huyo mdai wake yupo hapo ofisi za mtandao huu, lakini alitakiwa ajibu tu madai yanayomkabili siyo kujua huyo mtu yupo au la matokeo yake Jane hakuwa muwazi kwani hakuweza kukubali wala kukataa.
Mtandao huu unakuhaidi kufuatilia kwa undani suala hili na kisha kukuletea taarifa kamili juu ya sakata hili.
Post a Comment