HAKIGRAM IKITUMIKA IPASAVYO ITAWANUFAISHA WASANII
Naungana na serikali kupitia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, alipokuwa anajibu swali Mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya (CCM) mjini Dodoma Julai 27, 2011.
Ni ukweli kwamba, utaratibu wa kila msambazaji kuingia mkataba na msanii kusambaza idadi flani ya nakala na kupewa stika za HAKIGRAM ambazo zitabandikwa kwa kila nakala kutawezesha kujua msanii kauza nakala ngapi na kwa muda upi.
Kazi nyingi za wasanii wa Tanzania zinauzwa kinyume na sheria nchi za Congo , Burundi , Malawi , Rwanda na Zambia .
Waharamia wa kudurufu kazi za wasanii wametajirika huku wahusika wakiwa katika hali ya umasikini na wanafanya bila uoga kutokana na kosekana kwa sheria ya kuwabana moja kwa moja.
Nasema hivyo nikiwa na ushahidi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama ambaye amekuwa akipambana na maharamia hawa kila kukicha.
Hivi karibuni Msama alifanikiwa kukamata mtambo mmoja mkubwa wa kudurufu CD wenyewe uwezo wa kuzalisha CD feki 300 ndani ya dakika 20.
Na ili zoezi hili lifanikiwe inatupasa waimbaji wote wa muziki wa Injili na wadunia kuungana kwa pamoja ili kuondoa ujangili huu ambao unadidimiza maisha ya wasanii huku wasiohusika wakitajirika.
Mpaka sasa Msama amefanikiwa kuwakamata baadhi ya wanyonyaji kama Fred Jumbe, Martin Mkinga na Mstafa Rashidi.
Post a Comment