KUZAMA KWA MELI ZANZIRBAR ZOEZI LA KUOKOA MIILI YA MAREHEMU LINAENDELEA ENEO LA TUKIO
Zoezi la kuokoa miili ya marehemu waliopoteza maisha jana kwale ajali ya meli iliyokuwa imewabeba takriban watu zaidi ya 250 linaendelea kufanywa na jeshi la wanamaji nchini.
Miili kadhaa imezidi kuokolewa ndani ya Bahari ya Hindi baada ya zoezi hilo kusitishwa jana kutokana na hali mbaya ya hewa na giza kuingia.
Idadi kamili ya watu waliopoteza maisha itatolewa leo na jeshi la polisi nchini ambapo mpaka sasa inakadiliwa maiti zaidi ya 50 zimepatikana.
Meli hiyo ilipigwa na dharuba ya upepo mkali katika eneo la Chumbe pindi ilipokuwa inatoka jijini Dar es Salaam kuelekea visiwani Zanzibar.
Itakumbukwa kwamba, ni takriban mwaka mmoja sasa tokea ajali ya meli iliyokuwa imezidisha mizigo katika pwani ya kisiwa cha Zanzibar ikiwa na watu takriban 800.
Septemba mwaka jana meli ya MV Spice Islanders ilipata ajali mwishoni na kusababisha vifo vya takriban watu 200 na majeruhi 619 ambao waliokopolewa. Meli hiyo ilibeba abiria 3,000 wakati uwezo wake ni kubeba abiria 600 tu.
Ajali ya meli inayoshika rekodi ya kuua watu wengi mpaka sasa ni MV Bukoba ambayo tukio hilo lilitikisa taifa la Tanzania na kusababisha mshituko kwa wananchi wengi. Ajali hiyo ilitokea Mei 21, 1996, katika Ziwa Victoria.
Meli hiyo ilizama umbali wa takribani maili 30 sawa na kiliomita 56 kutoka Bandari ya Mwanza ikiwa na abiria zaidi ya 1000.
Meli ya MV Bukoba ilitengenezwa mwaka 1979 na ilikuwa na uwezo wa kubeba tani 85 za mizigo na abiria 430. Siku ya ajali inaripotiwa kuwa meli hiyo ilikuwa na jumla ya abiria 443 katika vyumba vyake vya Daraja la Kwanza na Daraja la Pili; lakini haikujulikana idadi halisi ya abiria katika Daraja la Tatu.
PICHA KWA HISANI YA MITANDAO MBALIMBALI |
Post a Comment