LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

ANYWESHWA DAMU YA HEDHI NA MAMA YAKE

Wahenga walisema kuwa ‘Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni’. Si jambo la kawaida kwa mtu kunywa ama kula matapishi yake kwa hiyari yake lakini inawezekana kwa shinikizo la mtu hasa anayekuzidi uwezo na mwenye hila na wewe.

Kila mtu unayemuona anaingia kanisani na kuomba kwa bubujiko la Roho Mtakatifu ukafikiri moyoni mwake yu salama la hasha. Ni vigumu sana kujua siri aliyoibeba mtu moyoni mwake na si kila anayeingia kanisani kweli ni mcha Mungu.

Pia siyo kweli wanaosali makanisa ya kiroho hao ni wema. Hapa nakuletea mkasa wa kweli ambao umemkuta dada mmoja aitwaye Ester aliyenyweshwa damu yake ya hedhi na mama yake wa kambo ambaye ni mlokole mzuri katika kanisa moja mjini Arusha.

Akizungumza na TGM hivi karibuni ndani ya Huduma ya The Word of Reconciliation Ministries jijini Dar es Salaam, Easter alisema kuwa, wazazi wake  walimfanyia kitendo hicho kwa tamaa ya kumiliki mali.
“Baba na mama waliamua kunifanyia hivyo kwa lengo la kunipumbaza akili ili niwe ndondocha na wao wawe matajiri,” alisema.
Easter alisema kuwa, siku ya tukio alitoka ndani kwa lengo la kutupa uchafu baada ya kupata siku zake (hedhi) lakini alistaajabu mama yake huyo wa kambo alipomfuata na kumzuia ili arudi ndani.
“Nilipoingia ndani aliniuliza nimebeba nini mkononi, nikamwambia sina kitu, cha kushangaza aliniambia niuchukue uchafu huo kisha niikamulie damu hiyo kwenye kikombe alichonipa,” alisema Easter huku machozi yakimtoka.
Dada huyo aliendelea kueleza kuwa, baada ya kuikamulia damu hiyo kwenye kikombe, aliambiwa aendelee na kazi zake. Kesho yake asubuhi aliitwa chumbani kwa mama yake na kulazimishwa kuinywa damu hiyo.
Baada ya kuinywa alipoteza fahamu na alipozinduka alijiona akiwa tofauti na siku nyingine. Tangu siku hiyo alikuwa anatokwa na damu kila sehemu yenye uwazi.

Kwa leo naishia hapa usikose kuufuatilia kesho ambapo utaona jinsi Easter alivyonusurika kupelekwa mochwari baada ya kupoteza fahamu kwa siku nne mfululizo.
Pia utaona ulokole wa mama yake aliyempaka mafuta sehemu za siri akidai ni ya upako baada ya kupewa maagizo na mchunguji wake wa kanisa moja huko Arusha.

Newer Post Older Post