CHRISTINA MATAI KUKAMILISHA ALBAMU YAKE MPYA
Baada ya ukimya wa muda mrefu mwambaji wa muziki wa Injili nchini Christina Matai (Mwang'onda) ‘The Tanzanite Lady’ kwa sasa yupo katika hatua za mwisho za kukamilisha albamu yake ya nne ikiwa katika mfumo wa CD. Albamu yake ya kwanza ilijulikana kwa jina la Yesu Ni Nani yapili ni
Mumgu Upo na ya tatu ni
Sinto Rudi Misri
Akizungumza na TGM leo asubuhi, The Tanzanite Lady’ alisema kuwa akishakamilisha albamu hiyo atawaambia mashabiki wake nini kinachoendelea. Mwimbaji huyo alianza kuimba nyimbo za injili mnamo mwaka 1998 akiimba katika kundi lililofahamika enzi hizo The Winnas.
Mwaka 2004 alitoa albamu yake ya kwanza akiwa nje ya kundi iliyoitwa Yesu Ni Nani.
Christina ni muasisi wa nyimbo za injili katika mahadhi ya taarab, wimbo wake wa kwanza uliojulikana kama Ujumbe Kwa Wanawake wenye asili ya taarabu ulimfanya awe mwanamuziki wa kwanza kuimba wimbo wenye miondoko ya mwambao wa pwani.

Mbali na uimbaji mwana mama huyu pia ni mfanyakazi na ana watoto wawili aliozaa na marehemu mume wake Mwang’onda ambao ni wakike na wakiume.
Post a Comment