SAUTI ZA SIFA KUWEKA HISTORIA MATEMBELE YA PILI KIVULE
Kwaya ya nyimbo za kusifu na kuabudu ya Huduma ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM) iliyopo Matembele ya Pili Kivule inatarajia kuweka historia ya kipekee Jumamosi hii itakapokuwa inazindua albamu zao mbili kwa pamoja.
Akizungumza na TGM leo jijini Dar es Salaam, mwalimu wa kwaya hiyo, Elibariki Isango alisema katika uzinduzi huo utakaoanza saa 6:00 mchana waimbaji kama Miriam Lukindo Mauki na Christina Shusho waimba kwa kupokezana na hakutakuwa kiingilio.
“Namshukuru Mungu Miriam amekubali kuja kutuunga mkono katika shughuli yetu ya kuzindua albamu zetu mbili na ataungana na Shusho ambaye naye amethibitisha kuwa nasi siku hiyo hivyo naomba wakazi wote wa Dar es Salaam na vitongoji vyake kufika kwa wingi kwenye uzinduzi huo,” alisema Isango.
Isango aliendelea kusema;“Tunatarajia kuweka historia ya kipekee siku hiyo kwani kuna waimbaji wengi ambao hawajawahi kuimba Matembele ya Pili ukichangana na mazoezi tuliyofanya hakika naamini kila atakayefika siku hiyo hatajuta kupoteza muda wake kwani Shusho na Miriam watakuwa wanapokezana kupanda jukwaani.”
Isango alisema kuwa lengo la uzinduzi wa albamu hizo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la huduma hiyo ambalo kwa sasa lipo katika hatua za mwisho hivyo kila atakayefika katika uzinduzi huo na kununua CD zao atakuwa ametoa sadaka yake ya kukamilisha hekalu la Bwana.
Mbali na Miriam na Shusho, waimbaji wengine watakaoimba kwenye uzinduzi huo ni Ami Mwakitalu, Madamu Luti & Chris, Faraja Moleli, Queen Talaba, Wilson John, Magreth na wengine wengi.
Mwalimu Isango alimaliza kwa kuwataka wadau wa muziki wa injili hasa wanaoishi maeno ya Kitunda, Ukonga na Gongolamboto kufika kwa wingi kwani hiyo ni mara ya kwanza kwa waimbaji kama Shusho na Miriam kuimba eneo hilo.
Post a Comment