UTAFITI WA UMOJA WA WAIMBA INJILI TANZANIA
Hivi karibuni niliandika juu ya suala la kukosekana kwa umoja ndani ya waimba injili na kutaja baadhi ya makundi ambayo yamekuwa yakijitenga yanapotoa huduma.Si mimi wa kwanza kuona hali hiyo bali jambo hili linasemwa na watu wengi akiwemo Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Stara Thomas ambaye aliliona hilo baada ya kuingia katika muziki huo.Baada ya kutoa maoni yangu haya katika blog hii kwa lengo la kujenga na kuondoa makundi haya, kuna mpendwa mmoja ameibuka na kusema hakuna hali hiyo na kunitaka nifanye utafiti wa kutosha kabla ya kuandika jambo kama hili.Nii imani yangu kuwa, sipo hapa kwa ajili ya kubomoa huduma za watu isipokuwa kujenga na siku zote mtu anayesema kweli lazima aonekane anamatatizo.Siwezi kushangaa maoni ya msomaji wangu wa blog hii lakini akumbuke ukweli ndiyo huu. Na haya ndiyo maoni ya msomaji wangu.
Anonymous said...
fanya utafiti sio unakurupuka kuwakilisha mawazo yako kwa sababu zako za msingi. kuna sababu ya msingi ya kusema kuna makundi wakati wengine uliowaweka ktk makundi tofauti wamekua wakifanya tour/matamasha pamoja mara kadhaa.nafkiri una sababu zako,na wewe ndio unataka makundi yawepo. watu pengine wamezoeana ndo maana wanafanya kazi pamoja,au wana sali pamoja na si lazima wanamuziki wote wawe wanajuana na kuzoeana kiasi cha kufanya kazi nying pamoja.pengine sababu ya kutofanya kazi pamoja ni kwamba hawajuani,na once wakikutanishwa watafanya tu kazi pamoja.angalia kwa makini,chunguza ndo uandike si kukurupuka kisa una kjukwaa la kupotosha watu
Wewe mudau unasemaje juu ya suala hili? Uwanja ni wako – By George Kayala.
Post a Comment