ALA CHUNGWA, APOTEZA FAHAMU
Kijana mmoja
aliyefahamika kwa jina la Pascal Raphael mwanafunzi wa shule ya sekondari ya
Tarime mkoani Mara amekutwa akiwa hajitambui nyumbani kwa kaka yake
aliyejulikana kwa jina la Edward mkazi wa Yombo baada ya kupoteza fahamu
kutokana na kula kipande cha chungwa alilopewa na bibi yake.
Habari kutoka
eneo la tukio zinasema kuwa Pascal alikutwa amelala nje ya geti la nyumba ya
kaka yake akiwa amezungushiwa majivu na katika paji lake la uso alikuwa na
maandishi ya rangi nyekundu yakiwa yameandikwa kwa lugha ya kiarabu na katika
kumpekua alikutwa na nyembe, nywele na vitu mbalimbali kana kwamba amelukwa
akili.
Kabla ya
tukio hilo kijana huyo alisafirishwa na kaka yake kwenda kijiji kwao Tarime
baada ya kushindwana kitabia tangu mwezi wa pili mwaka huu na kushangazwa na
kitendo cha kumkuta nyumbani hapo akiwa katika mazingira hayo.
Kijana huyo
baada ya kuamushwa alikuwa hajiwezi hata kuongea ilikuwa shida mpaka akapelekwa
kwa mtumishi wa Mungu akafanyiwa maombi kasha fahamu zake zikarejea na kuanza
kusimulia kilichomkuta kabla ya kufika hapo.
Pascal
alisema kuwa Ijumaa iliyopita akiwa kijijini kwao alichukua fedha na kwenda
benki kulipia ada ya shule na kasha kurudi nyumbani na alipofika nyumbani
alimwambia bibi yake kuwa anajisikia vibaya ndipo bibi huyo akampa chungwa na
kumwambia ale.
Kijana huyo
aliingia ndani na kukata kipande hicho cha chungwa mara akaanza kusikia kizunguzungu
na kuona giza nene na kupoteza fahamu na yeye alishanga kuzinduka akiwa
nyumbani kwa kaka yake akiwa katika mazingira hayo.
Kitu kingine
kilichomshangaza Pascal ni kutokuwa na nywele zake alizokuwa nazo kabla ya
tukio hilo na mpaka sasa haelewi chochote.
Post a Comment