KANISA LAFUNGWA BAADA YA WAMASAI KUTOA KIPIGO
Mkuu wa wilaya ya Kilindi Selemani Liwowa |
Kanisa moja mkoani Tanga limefungwa baada ya Wamasai wa
Songe mkoani Tanga kutembeza kipigo kwa wamuumini wa kanisa hilo kwa madai kuwa
linapinga mila potofu kama kuacha kuwakeketa wanawake na wanawake wa kimasai
kuolewa na jamii isiyokuwa yao.
Askofu wa kanisa hilo Daniel Lekonga amesema kuwa wamasai
hao wameamua kutembea kipigo hicho na kuiba vifaa vya kanisa hilo huku baadhi
ya wachungaji wa waumini wakijeruhiwa. Askari wa jeshi la polisi Songe walifika
katika eneo la tukio na kukamata mtu mmoja hali iliyosababisha kundi kubwa la
kimasai liandamane mpaka kituoni hapo kwa shinikizo la kumtoa mwenzao.
Habari kutoka katika eneo la tukio zinasema kuwa wamasai hao
wamefanikiwa pia kumrejesha kwao msichana mmoja wa kimasai aliyeolewa na
mwanaume asiye masai kwa kile walichodai kuwa kufanya hivyo ni kukiuka mira
zao. Mwanaume aliyemuoa mwanamke huyo alipata kipigo na kukubali kuachana naye.
Mkuu wa wilaya ya
Kilindi Selemani Liwowa, amethibisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kuwa ugomvi huo ni mkubwa hivyo wanataka kuzikutanisha
pande zote mbili ili wajue kwa undani zaidi tatizo lipo wapi na kufanya eneo
hilo liwe salama.
Post a Comment