BARAKA KUACHANA NA UKAPELA MWEZI AGOSTI
Baraka |
Mwimbaji wa nyimbo za injili jijini Dar es Salaam anatarajia
kuachana na ukapela baada ya kumpata mke mwema kutoka kwa Mungu aitwaye Mary
Jastin mkazi wa mkoa wa Mbeya. Akizungumza na Tanzania Gospel Music leo hii,
Baraka alisema kuwa harusi itafungwa katika kanisa la Church of God lililopo
Mbeya. “Kila kitu kwa ajili ya maandalizi ya harusi yangu kinaenda vizuri na
sasa nasubiri siku ifike nimchukue mke wangu mpenzi toka kwa Mungu na ni tukio
ambalo nilikuwa nalisubiri kwa shauku kubwa katika maisha yangu,” alisema
Baraka. Baraka aliendelea kusema kuwa tukio hilo anatarajia litakusanya umati
mkubwa wa ndugu na marafiki wenye mapenzi mema katika maisha yake. Habari kamili
juu ya harusi hiyo endelea kufuatilia mtandao huu.
Post a Comment