CHAPANYOTA: JULAI 21 ITAKUWA SIKU YA KUKUMBUKWA MBEYA
Mwimbaji wa nyimbo za
injili nchini, Ambele Chapanyota amesema kuwa Julai 21, 2013 itabaki kuwa siku
ya kukumbukwa kwa wakazi wa mkoa wa Mbeya ambapo ataimba vibao vyake vyote na
vingine ambavyo havijawahi kusikika popote pale katika uzinduzi wa DVD ya
Nitang’ara Tu ya Mwinjilisti Kabula George.
Chapanyota mwenye maono
ya kuibadilisha jamii ya Tanzania kwa njia ya uimbaji na kuhubiri neono la
Mungu alisema kuwa kwa sasa anafanya maandalizi makali yeye na vijana wake
ambao wamekuwa wakilitawala jukwaa kwa nguvu zote.
“Julai 21, 2013
itabakiwa siku ya kukumbukwa kwa wakazi wa Mbeya watakaofika katika uzinduzi wa
Mwinjilisti Kabula utakaofanyika katika Kanisa la Moravian Usharika wa
Yerusalem maeneo ya Airport kwani kuna vitu vikali ambavyo sijawahi kuvionesha
popote pale siku hiyo nitavionesha,” alisema Chapanyota.
Chapanyota amewataka
wakazi wote wa mkoa wa Mbeya siku hiyo kufika kwa wingi katika uzinduzi huo
ambao ni wa kwanza kufanywa na mwinjilisti Kabula hivyo ni vema wakaonesha
ushirikiano wa kujumuika kwa pamoja kwa ajili ya kufanikisha shughuli hiyo.
Mwimbaji huyo
anayetamba na albamu zake mbili SALAMA KWA YESU na YESU TU amemaliza kwa
kusema kuwa siku hiyo siyo ya kukosa kwani hatapenda kuona mtu anasimuliwa kile
atakachokifanya katika ukumbi huo.
Post a Comment