LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

ROSE MUHANDO: MWAKA HUU LAZIMA NIOLEWE


Rose Muhando
Hii imekaa vizuri. Malkia wa nyimbo za injili nchini, Rose Salum Mhando amesema kuwa mwaka huu hautapita bila kuolewa na sasa tayari anayemchumba wake ambaye atamtambulisha kwa wadau siku si nyingi.
Akizungumza na Tanzania Gospel Music hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Rose alisema kuwa, kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na watu kwa kutaka kujua kwa nini haolewi bila wao kujua kwamba kila jambo linawakati wake.
“Watu wengi wamekuwa wakiniuliza lini nitaolewa kwani huduma yangu inapendeza nikiwa na mume lakini hawaju kuwa kila jambo lina wakati wake. Namshukuru Mungu tayari mchumba ninaye na siku si nyingi nitamtangaza hadharani,” alisema Rose.
Rose alisema kuwa, kwa muda mrefu amekuwa akisingiziwa kutoka kimapenzi na wanaume mbalimbali kitu ambacho kimekuwa kikimkwasa sana kwani kila mwanaume anayeonekana anaukali naye wanahisi anatoka naye kimahaba.
“Hakuna mwanamke asiyependa kuolewa. Hata mimi napenda sana lakini siwezi kulazimisha kama wakati haujafika. Lakini Mungu ni mwema kwangu wakati sasa umefika,” alisema Rose.

Rose amezaliwa 1976 katika kijiji cha Dumila, wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro. Kabla hajawa mkristo alikuwa Muislam na ni mama wa watoto watatu. Mwimbaji huyo alimpokea Yesu Kristo baada ya kuugua kwa muda mrefu na akawa  kitandani akiwa na umri wa miaka 9.  Mtumishi huyo wa Mungu  aliugua kwa muda wa miaka mitatu na uponyaji wake ulitokana na maombezi na ndipo akaamua kubadili dini.

Kabla ya kuwa mwimbaji binafsi, Rose alikuwa  katika kwaya iliyoko Dodoma na alikuwa mwalimu wa Kwaya katika kwaya ya Dodoma St. Mary's katika kanisa la Kianglikana la Chimuli.

Newer Post Older Post