WATOTO WAWILI WAFA BAADA YA KUTUMBUKIA CHOONI
Watoto wawili
mmoja miaka mitatu na mwingine miaka minne wamefariki dunia baada ya kutumbukia
kwenye shimo ambalo limechimbwa kwa ajili ya matumizi ya choo likiwa na futi 12
na lilikuwa limejaa maji machafu.
Tukio hilo
limetokea juzi mkoani Mara ambapo watoto hao walikuwa wakicheza majira ya jioni
na walikuwa wakicheza kwa kukimbizana na watoto wenzao na shimo hilo lilikuwa
limefunikwa kwa majani ambayo yaliwafanya marehemu hao wasijue kama kuna kitu
hicho na kukuta wanazama ndipo rafiki zao wakaenda kutoa taarifa kwa watu
waliokuwa jirani.
Watoto hao
waliokolewa wakiwa wamekunywa maji mengi na kukimbizwa hospitali lakini
walifariki wakiwa njia.
Jeshi la
Polisi mkoani hapo limethibitisha kutokea kwa kifo hicho na hakuna
anayeshikiliwa kutokana na tukio hilo kwani mmiliki wa nyumba yenye shimo hilo
ni mzee ambaye hakuwa na uwezo wa kukiendeleza choo hicho ambacho kiliachwa na
ndugu yake ambaye alifariki siku nyingi na kumuacha peke yake.
Post a Comment