LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

KAMPENI YA KOMESHA UCHAWI NA MCHAWI LETA ROHO KWA YESU Umati mkubwa wa watu wafunguliwa nguvu za giza *Wachawi watajana mbele ya madhabahu *Wakiri kuelemewa na nguvu ya Mungu kupitia Nabii na Askofu Suguye


Dada huyo ambaye jina lake halikujulikana mara moja akilia kwa uchungu wakati wa maombezi ya kukomesha uchawi.
Jumapili iliyopita itabaki kuwa ya historia kwa umati mkubwa wa waamini waliofika katika huduma ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM) baada ya wachawi kuanza kutajana waziwazi mbele ya madhabahu hiyo huku wengine wakikiri kuelemewa na nguvu ya Mungu kupitia Nabii na Askofu Nicolaus Suguye.
Wakizungumza na gazeti Tanzania Gospel Music jana  mara baada ya maombezi yaliyofanyika ibada ya kwanza naya pili chini ya Nabii na Askofu Suguye waamini hao walisema kuwa kampeni hiyo iwe ya kudumu kwani imeonekana kuwa mkombozi kwa watu wengi walioteswa na shetani kwa muda mrefu.
“Hii itabaki kuwa historia kwa wakazi wa Kivule hasa waaamini wa huduma hii ya WRM kuona wachawi wakitajana waziwazi mbele ya madhabahu juu ya kazi wanazozifanya nyakati za usiku na kufunga maisha ya watu mbalimbali,” alisema mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maria Mwaibale.
Naye Joseph John alisema kuwa ametembea katika huduma nyingi lakini hajawahi kukutana na nguvu ya Mungu kama aliyoiona WRM nay eye binafsi alifunguliwa nguvu za giza ambazo zimekuwa zikimtesa kwa muda mrefu.
“Muda mrefu nilikuwa namsikia Nabii Suguye kupitia vyombo vya habari juu ya nguvu ya Mungu aliyonayo juu ya watu waliofungwa na nguvu za giza. Niliposikia kampeni hii niliamua kufika kuona kama kweli naweza kufunguliwa vifungo vyangu, hakika kweli huyu ni mtumishi wa Mungu aliyeitwa kwani niko huru kabisa,” alisema John.
Tangu kampeni hiyo ianze mwezi uliopita shuhuda za watu wengi wanaofunguliwa nguvu za giza zimekuwa nyingi na Jumapili iliyopita ilikuwa na aina yake kwani wachawi wengi waliumbuka kwani walikuwa wanatajana huku wengine wakiaga na kusema kampeni hiyo imefanikiwa kuharibu kazi zao.
Kampeni hiyo inaendelea tena kesho Jumamosi chini ya Nabii Suguye na Manabii wadogo na watenda kazi wengine kuhakikisha watu wanafunguliwa nguvu za giza na kuharibu maisha yake.

Newer Post Older Post