LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

KAMPENI YA KOMESHA UCHAWI NA MCHAWI LETE ROHO KWA YESU WACHAWI WAZIDI KUUMBULIWA WRM *Mtoto aliyechukuliwa sehemu zake za siri k wa njia ya kichawi aombewa na kurejeshewa *Mama yake mzazi asimulia jinsi alivyotabika baada ya mkasa huo

Waamini wa WRM wakisikiliza ushuhuda wa mama (pichani hayupo) ambaye mwanaye sehemu zake za siri zilichukuliwa kichawi

Kampeni ya Komesha Uchawi na Mchawi Lete Roho kwa Yesu inayoendelea katika Huduma ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM) nchini ya Askofu na Nabii Nicolaus Sugure imezidi kuwauumbua wachawi baada ya awamu hii kurejesha sehemu za siri za mtoto anayekadiliwa kuwa na mwaka mmoja kupotea kimiujiza.
Akizungumza na Tanzania Gospel Music hivi karibuni ndani ya WRM Jumapili iliyopita, Koreta Soso ambaye ndiye mama mzazi wa mtoto Siloam Steven Soso alisema kuwa mwanaye alimzaa akiwa kawaida na wiki mbili zilizopita ndipo alipata kituko hicho ambacho kiliwashangaza watu wengi.
“Mwanangu nilimzaa kawaida lakini wakati kampeni hii inaendelea katika huduma ya WRM ndipo kilitokea kituko hiki cha mwanangu kupoteza sehemu za siri za kutolea haja ndogo na kuonekana kana kwamba alizaliwa hivyo.
“Tukio hilo lilinikosesha raha nikaamua kwenda hospitali ya Kivule nao wakasema mtoto huyo anatakiwa kufanyiwa upasuaji na kutakiwa kwenda Amana. Kabla ya kwenda Amana nikakumbuka kuwa kuna kampeni ya kukomesha uchawi na mchawi WRM ndipo nikaamua kumpeleka,” alisema Koreta.
Koreta aliendelea kusema kuwa baada ya kufika WRM aliwakuta watenda kazi na kuwasimulia tukio hilo nao wakamwangalia na kushtushwa na tukio hilo kwani mtoto huo hakuwa hivyo siku za nyuma.
Mama Siloam alifika kwa Askofu na Nabii Suguye na kufanyiwa maombi kisha akaambiwa kuwa aende Amana na akifika huko asikubali kufanyiwa chochote kwani tayari Bwana ameshafanya.
Mama huyo aliendelea kusema kuwa alipofika Amana madakitari walipomuangalia wakasema anatakiwa kufanyiwa upasuaji haraka na kuitwa daktari wa upasuaji lakini katika hali ya kumtukuza Mungu wa WRM wakati daktari anafanya ukaguzi sehemu hiyo ya siri ikaonekana.
Huyo ndiye Mungu wa WRM ambaye anafanya miujiza ya ajabu kwa kuwaumbua wachawi jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo iliendelea Alhamis na jana Jumamosi na leo inaendelea kwa lengo la kuwakomboa watu wanaoteswa na nguvu za giza.

Newer Post Older Post