TAMASHA KUBWA LA INJILI LAANDALIWA MBEYA
Tamasha
kubwa la muziki wa injili limeandaliwa
na mwimbaji wa nyimbo za injili nchini
Mwinjilisti Kabula George na litafanyika
katika kanisa la Moravian Usharika wa Yerusalem Air Poirt Mbeya mjini Julai 21
mwaka huu na litaenda sambamba na kuizindua kwa mara nyingi DVD yake ya albamu
ya Nitang’ara Tu.
Akizungumza na Tanzania Gospel Music leo
jijini Dar es Salaam, Mwinjisti Kabula alisema kuwa ameamua kuaandaa tamasha
hilo kutokana na wakazi wa jiji hilo
kuomba aandae tamasha hilo kutokana na kuzipenda nyimbo zake ambazo zimekuwa
zikiwagusa kila wanapozisikiliza redioni.
“Nimeandaa
tamasha hilo mkoani Mbeya baada ya
kupokea maombi ya wakazi wengi wa Nyanda za Juu Kusini nami nimeona nikubali
ombi lao na taratibu zote kwa ajili ya tamasha hilo yanaendelea hivyo naamini
wakazi wa mkoa huo watapata kile wanachokitaka,” alisema Mwinjilisti Kabula.
Mwimbaji
huyo alisema kuwa tamasha hilo litakuwa na waimbaji wengi kutoka mikoa
mbalimbali kama Njombe, Dar es Salaam na wenyeji Mbeya na kuahidi kuacha
histoaria nyanda hizo.
“Litakuwa tamasha
la kipekee kufanyika katika mkoa huo kwani litawakutanisha waimbaji nyota
kutoka katika mikoa mitatu ambayo ni Njombe, Dar es Salaam na wenyeji Mbeya
hivyo si siku ya kukosa,” alisema Mwinjilisti Kabula.
Mwinjilisti
Kabula alisema pia kuwa siku hiyo kwa mara ya kwanza ndipo ataziuza DVD zake
kwa mashabiki wote watakaofika katika uzinduzi huo na anaamini kila mmoja
ataondoka na nakala yake halisi.
Post a Comment