ASKOFU SUGUYE ASIMULIA JINSI MUNGU ALIVYOMPONYA NA KIFO
Askofu wa Huduma ya Neno la Upatanisho(The Word of Reconciliation Ministries) iliyopo Busitani ya Edeni Kivule zamani Matembele ya kwanza, Nicolauc Suguye ameelezea jinsi Mungu alivyomwepusha na kifo, baada ya kutoakea ajali mbaya ya basi la Taqwa Novemba 21 mwaka huu Dodoma na kuua watu wawili huku gari hilo likiteketea kwa moto mbele ya macho yake na mkewe Anna Suguye.
Akisimulia kisa hicho, Askofu ambaye yeye na mkewe walikaa kiti cha nyuma ya dereva ambaye alitekea na moto palepale, kabla ya kufunga safari ya kuelekea nyumbani kwao Ngala, walioteshwa suala la matukio ya dalili za roho ya mauti, huku mkewe akiona kwenye ndoto majeneza mawili yakiwe wamewekwa mbele ya kanisa, na alipoamka asubuhi alipuuza ndoto hiyo na kuona kama ni jambo la kawaida, kwa sababu suala la kuota ndoto za ajabu si geni kwake.
Askofu alisema kuwa, wakiwa kwenye gari, dereva na kondakta walikuwa wanaongea maneno ambayo kwa kiasi fulani hayakupaswa kuzungumzwa wakati gari likiwa kwenye mwendo mkali, na mara nyingo Suguye alijaribu kumuonya dereva asiendelee kuongea wakati gari likiwa barabarani.
Hata hivyo, wahenga walisema sikio la kufa halisikii dawa, dereva huyo aliendelea kupiga stori na konda wake na mbele yao kulikuwa na basi la Zuberi lililokuwa linaelekea Mwanza, na kutokana na mwenda wa gari lao kuwa na mwendo mkali, lilijaribu kulipita basi la Zuberi wakati huo dereva alikuwa bado anaendelea kuongea, na kondakita wake.
Wakati anajaribu kuripita basi hilo, kondakita alionekana kumpa kitu dereva wake na alipogeuka kukichukua mara mbele yake aliona trekita likiwa karibu yake, na alipotaka kulikwepa gari lilianza kuyumba na mara taili moja iliingia kwenye korongo lililokuwa barabarani na ndipo lilipopasuka upande wa dereva na kuangukia upande wa pili.
Kitendo cha kupiduka kwa gali hilo, kulimfanya ajikute nje ya gari akiwa anatoka damu kichwani, na mara alisikia sauti ya mke wake ikiuliza "mme wangu uko wapi", na katika hali ya kushangaza, mke wake naye alijikuta yupo nje pasi kufahamu alifikaje lakini yeye hakuumia sana mbali na kupata jeraha dogo kwenye goti.
Askofu alimaliza kwa kusema kuwa, siku hiyo malaika wa Bwana walikuwa upande wao kwa sababu jinsi walivyotoka kwenye basi hilo hawakujua licha ya kuumia kichwani na kushonwa nyuzi tatu na Jumapili ijayo Desemba 06, atatoa sadaka ya shukurani kanisani hapo.
One Response to “ASKOFU SUGUYE ASIMULIA JINSI MUNGU ALIVYOMPONYA NA KIFO”
I want to thank GOD very much for saving Bishop Nicolus Suguye and Pator Anna Suguye of WRM.
Infact this was remarkable accident of the year 2009, which claimed two life on spot.
I actually attended the service of thanks giving and there more than enough reason to thank God for what He had done.
I dont need to go back to the story but beleive these words that GOD sent an angle from heaven to bring these two servants of God out of that terifying accident, its was not easy to escape the openned grave, but only Jesus did what was deservable.
I just call upon every person to keep on praying for servants of GOD wherever they are, because satan always targets them so much, for the WORD says I WILL HIT THE SHEPHERDS AND FLOCKS WILL SCARTER"
May GOD help our spiritual leaders so much.
Be blessed
Servant in House of GOD.
Post a Comment