NYIMBO ZA KABULA ZAZIDI KUWA BARAKA KWA WATU WENGI
Nikama hadithi, lakini ni kweli kuwa nyimbo za muimbaji wa muziki wa Injili nchini Kabula J.George zimeendelea kufanyika baraka katika jamii baada ya siku za hivi karibuni Askofu wa Huduma ya Neno la Upatanisho (The Word of Reconciliation Ministries), Nicolaus Suguye (pichani) na Michael Lucas Mkenda kuelezea jinsi nyimbo hizo zilivyowahudumia baada ya kupatwa na matatizo.
Mkenda yeye hivi karibuni alikamatwa na jeshi la polisi nchini baada ya kudai kuiba mali yenye thamani ya shilingi bilioni moja na kujikuta anapata mateso makali kutoka kwa askari waliokuwa wamemkamata wakifanya hivyo kwa lengo la kumbana akiri kuwa yeye ndiye aliyechukua mali hiyo vinginevyo watamuua.
Baba huyo aliteswa vikali na askari hao ambao inasadikika kuwa walipewa pesa na mwenye mali ili wamtese na kweli walifanya hivyo na walimkaba shingo mpaka haja ndogo ikatoka lakini yeye alivumilia kwa kujua kuwa mateso aliyokuwa anayapata yalitokana na kuonewa na mwenye mali ambaye inadaiwa kuwa yeye ndiye aliyesababisha upotevu wa mali hiyo na kuamua kumtoa kafara ili aendelee kula vya wizi.Kwa habari kamili gonga hapa
Post a Comment