Nyimbo za Injili zenye uvuvio wa nguvu ya Mungu zinauponyaji
Kheri ya Krismasi mpenzi msomaji wa blog hii, namshukuru Mungu kwa kutufikisha siku hii kwani wengi wameshindwa kufika baada ya kupoteza maisha
Wiki hii aliyetawala katika safu hii ni Mtumishi wa Mungu mwenye kipaji cha hali ya juu Kabula George ambaye Mungu amekuwa akijidhihirisha kwa wanadamu kupitia nyimbo zake ambazo zimekuwa zikiwaponya watu waliofungwa na nguvu za
Kabula ambaye kwa sasa anatamba na albamu yake mpya ya Ushindi alisema kuwa, anamtukuza Mungu kwa kumtumia kadri awezavyo kwa sababu amekuwa akipata mialiko kutoka kila pembe ya nchi na awapo sehemu husika, Jehova hujidhihirisha kwa kuwaponya na kuwapa matumaini watu waliokata tamaa ya maisha na kuwaacha watu wakishindwa kuamini.
“Nina kila sababu za kumrudishia heshima na utukufu Mungu wangu kwa kujidhihirisha katika huduma yangu ambayo nimekuwa nikialikwa. Watu wengi wamekuwa wakipokea uponyaji pindi ninapokuwa naimba ama kuzisikiliza nyimbo zangu kwenye CD, kuziona kwenye VCD na DVD.
Hivi karibuni nilialikwa kwenye huduma moja jijini
Ghafla nguvu yenye upako wa aina yake ilishuka nikajikuta napiga magoti bila kutegemea na kuanza kububujikwa na machozi mara kila aliyekuwa kwenye huduma hiyo alishukiwa na nguvu hiyo na wote tukaanza kuomba.
Sikupata nguvu ya kunyanyuka, lakini Askofu wa Huduma hiyo Nicolaus Suguye ambaye naye alizama kwenye mambo, alipata alisimama na kuanza kuwaombea watu wenye shida mbalimbali. Siku hiyo taratibu zote za ibaada hazikufanyika, kwani askofu hakuhubiri tena kwa sababu watu walikuwa tayari wamezama kwenye maombi.
Baada ya huduma hiyo, mama mmoja aliyekuwa na uvimbe wa siku nyingi sehemu za siri alisimama na kushuhudia kuwa, wakati ninaimba ghafla alisikia nguvu inamshukia na kujikuta anaanguka chini bila kujitambua, na aliposimama uvimbe wote ulitoweka na sasa anaendelea na shughuli zake
Kabula alisema kuwa, anashuhuda nyingi
Mtumishi huyo wa Mungu alisema kuwa, siri ya nyimbo zake kuwa tiba kwa watu wenye matatizo ni kutokana na nyimbo zake kuwa na uvuvio wa nguvu za Mungu ambazo watu wengi wametokea kuzipenda baada ya kubaini kuwa, hakuna haja ya kwenda kuombewa na askofu, mwinjilisti, ama mchungaji pindi wanapozisikiliza katika roho na kweli na kuyaweka kwa vitendo maneno yaliyomo ndani ya nyimbo hizo.
“Nyimbo zenye uvuvio wa nguvu ya Mungu zinauponyaji, namshukuru
Kabula alimaliza kwa kusema kuwa; “Nyimbo zangu zinapatika kwa Mam Store atakayezihitaji kwa jumla na rejareja apige simu namba 0713328290, ama
One Response to “Nyimbo za Injili zenye uvuvio wa nguvu ya Mungu zinauponyaji”
naitwa Agnel, mwimbaji na msemaji wa RAFIKI GOSPEL SINGERZ.
Tumefurahi kuona taarifa zetu kwenye blogg yenu.
tunapenda kuwaona ili kushirikishana baadh ya mambo. Namba zetu ni 0712231595, 0712746398.
Hongereni sana.
Post a Comment