LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

Nyimbo za Injili zenye uvuvio wa nguvu ya Mungu zinauponyaji




Kheri ya Krismasi mpenzi msomaji wa blog hii, namshukuru Mungu kwa kutufikisha siku hii kwani wengi wameshindwa kufika baada ya kupoteza maisha yao kwa  njia ya ajali, ugonjwa na n.k.
Wiki hii aliyetawala katika safu hii ni Mtumishi wa Mungu  mwenye kipaji cha hali ya juu Kabula George  ambaye Mungu amekuwa akijidhihirisha kwa wanadamu kupitia nyimbo zake ambazo zimekuwa zikiwaponya watu waliofungwa na nguvu za giza kwa muda mrefu.
Kabula ambaye kwa sasa anatamba na albamu yake mpya ya Ushindi alisema kuwa, anamtukuza Mungu kwa kumtumia kadri awezavyo kwa sababu amekuwa akipata mialiko kutoka kila pembe ya nchi na awapo sehemu husika, Jehova hujidhihirisha kwa kuwaponya na kuwapa matumaini watu waliokata tamaa ya maisha na kuwaacha watu wakishindwa kuamini.
“Nina kila sababu za kumrudishia heshima na utukufu Mungu wangu kwa kujidhihirisha katika huduma yangu ambayo nimekuwa nikialikwa. Watu wengi wamekuwa wakipokea uponyaji pindi ninapokuwa naimba ama kuzisikiliza nyimbo zangu kwenye CD, kuziona kwenye VCD na DVD.
Hivi karibuni nilialikwa kwenye huduma moja jijini Dar es Salaam ijulikanayo kama Huduma ya Neno la Upatanisho (The Word of Reconciliation Ministries) na kupewa nafasi ya kuimba nyimbo mbili, kwanza niliimba  wimbo wa Hakuna Muweza ambao unasifu ukuu wa Mungu kisha nikamaliza na wimbo wa Dhihirisha ambapo nilimuomba Jehova adhihirishe uweza wake katika ya huduma hiyo.
Ghafla nguvu yenye upako wa aina yake ilishuka nikajikuta napiga magoti bila kutegemea na kuanza kububujikwa na machozi mara kila aliyekuwa kwenye huduma hiyo alishukiwa na nguvu hiyo na wote tukaanza kuomba.
Sikupata nguvu ya kunyanyuka, lakini Askofu wa Huduma hiyo Nicolaus Suguye ambaye naye alizama kwenye mambo, alipata alisimama na kuanza kuwaombea watu wenye shida mbalimbali. Siku hiyo taratibu zote za ibaada hazikufanyika, kwani askofu hakuhubiri tena kwa sababu watu walikuwa tayari wamezama kwenye maombi.
Baada ya huduma hiyo, mama mmoja aliyekuwa na uvimbe wa siku nyingi sehemu za siri alisimama na kushuhudia kuwa, wakati ninaimba ghafla alisikia nguvu inamshukia na kujikuta anaanguka chini bila kujitambua, na aliposimama uvimbe wote ulitoweka na sasa anaendelea na shughuli zake kama kawaida,” alisema Kabula.
Kabula alisema kuwa, anashuhuda nyingi sana ambazo amekuwa akipewa na watu wanaosikiliza nyimbo zake hasa wimbo wa Dhihirisha na Hakuna muweza ambazo zimeonekana kuwa tiba kwa watu waliofungwa na nguvu za giza.
Mtumishi huyo wa Mungu alisema kuwa, siri ya nyimbo zake kuwa tiba kwa watu wenye matatizo ni kutokana na nyimbo zake kuwa na uvuvio wa nguvu za Mungu ambazo watu wengi wametokea kuzipenda baada ya kubaini kuwa, hakuna haja ya kwenda kuombewa na askofu, mwinjilisti, ama mchungaji pindi wanapozisikiliza katika roho na kweli na kuyaweka kwa vitendo maneno yaliyomo ndani ya nyimbo hizo.
“Nyimbo zenye uvuvio wa nguvu ya Mungu zinauponyaji, namshukuru sana Mola kwa kuzivuvia nyimbo zangu nguvu yake, leo hii watu wanapata uponya, pasipo kwenda kuombewa katika mikutano ya dini ama makanisani,” alisema Kabula.
Kabula alimaliza kwa kusema kuwa; “Nyimbo zangu zinapatika kwa Mam Store atakayezihitaji kwa jumla na rejareja apige simu namba 0713328290, ama kama atanihitaji kwa ajili ya huduma awasiliane nami kwa simu namba 0757 140336.



Newer Post Older Post

One Response to “Nyimbo za Injili zenye uvuvio wa nguvu ya Mungu zinauponyaji”

Anonymous said...

naitwa Agnel, mwimbaji na msemaji wa RAFIKI GOSPEL SINGERZ.
Tumefurahi kuona taarifa zetu kwenye blogg yenu.
tunapenda kuwaona ili kushirikishana baadh ya mambo. Namba zetu ni 0712231595, 0712746398.
Hongereni sana.