UPORAJI MALI NA GHASIA VYASHAMILI HAITI
Wakati misaada zaidi ikiendelea kumiminika nchini Haiti kwa wahanga wa tetemeko la ardhi, vitendo vya uporaji na ghasia vimeshamiri katika mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo, Port-au-Prince, uliOpigwa na tetemeko hilo hivi karibuni.
Mamia ya watu waliokuwa na hasira ya kutokuwa na chakula walivamia maduka yaliyoharibiwa na tetemeko hilo na kupora bidhaa mbalimbali, huku wengine wakipigana kuwania bidhaa hizo.
Umoja wa Ulaya umetangaza msaada wa kiasi cha Euro nusu bilioni. Nalo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo linategemewa kuidhinisha pendekezo la kupelekwa kikosi cha askari wa ziada wa umoja huo 3,500 nchini Haiti katika kujaribu kukabiliana na matukio hayo ya uporaji.
Akizungumza mara baada ya kuzuru mji mkuu huo wa Haiti, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuwa wananchi wa Haiti wanahitaji msaada wa haraka.
Na inakadiriwa kuwa huenda idadi ya watu waliokufa kutokana na tetemeko hilo ikafikia watu laki mbili, huku maelfu kadhaa wakiwa hawana makazi.
Post a Comment