LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

Ayubu John; Dereva wa gari anayeendesha maisha kwa nyimbo za Injili

KATIKA miaka ya hivi karibuni, Muziki wa Injili umekuwa ni mkombozi kwa vijana na jamii kwa ujumla, hii ni kutokana na msaada wake katika kupunguza tatizo la ajira, pia ukitumika kama silaha ya kubadili tabia za wanajamii walio wengi.
Huduma hii imekuwa ikifanywa zaidi na vijana, imeendelea kuwa ni kiunganishi kikubwa baina ya jamii moja na nyingine hivyo kuchangia kujenga taifa imara lenye mwelekeo wa kumjua Mungu.
Ayubu John ambaye ni muimbaji wa nyimbo hizo, anasema kwamba kuna mambo kadhaa ambayo daima wanakuwa wakiyafanya kwa nia ya kuhakisha kuwa Tanzania na Afrika kwa ujumla inakuwa na mabadiliko kwa njia ya muziki wa Injili.
"Hii ni huduma muhimu katika kueneza Neno la Mungu, wapo watu wanaopokea ujumbe na kubadilika kwa njia tofauti ikiwemo, mahubiri Kanisani au kwenye mikusanyiko lakini wapo wengine wanaotegemea kupota ujumbe kwa njia ya uimbaji.
"Kwa sababu hii najiona kuwa mimi kama muimbaji wa nyimbo za Injili nina kazi ya ziada ya kuhakikisha kuwa jamii inayonizunguka inapata ukombozi na kubadilika kama ambavyo neno linavyosema," aliongeza Ayubu.
Muimbaji huyo ambaye kwa taaluma ni dereva, anasema kuwa katika maisha yake ya awali hakujua kuwa siku moja angweza kuja kuwa moja ya watu muhimu kwenye jamii ila siku moja Mungu alimuita ili amtumikie katika huduma hii.
Kazi yake alianza kufanya mwaka 2003 huku akieleza kuwa kulikuwa na vikazo vingi ambavyo aliamini kuwa vingeweza kumfanya ashindwe kuendelea mbele ingawa hakukata tamaa ila aliendelea kujituma kwa kuwa aliamamini kwamba ilikuwa ni sehemu ya maisha katika kumtumikia Mungu, kwa sababu hata Ibrahim baba wa imani na Ayubu washawahi kujaribiwa na walishinda majaribu hayo.
Tangu wakati huo aliendelea kufanya huduma hiyo, jambo lililomlazimu kuachana na kazi ya udereva ili kupata muda mwingi zaidi wa kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.
"Nimelazimika kuachana na kazi ya udereva ili niweze kufanya huduma yake kikamilifu, huu kwangu ulikuwa ni wakati mugumu maishani lakini kwa vile ulikuwa ni wito nililazimika kuukubali ingawa kwa sasa mambo yamebadilika kwa sababu Mungu amenibariki na kunipa kila ninachohitaji," ameongeza nyota huyo.
Kwa sasa Ayubu ana albamu mbili ambazo ni Nikifika Juu Mbinguni na Kesheni Mkiomba. Katika albamu ya kwanza imebeba jumla ya nyimbo kumi ambazo ni Nikifika Mbimbuni, Akili, Ni Hali gani, Yesu Nitakutukuza, Mungu Ulisema na Nikifika Mbinguni iliyobeba jina la albam.
Kazi ya pili nayo inajumla ya nyimbo 10, ambazo ni Acha Kulia, Mwenye Nyumba, Asante Yesu Asante Mungu na nyingine nyingi ambapo kwa sasa amehamishia makazi yake nchini Kenya katika jiji la Nairobi.
Akileelezea ujumbe wake kwa waimbaji wa Tanzania, Ayubu anasema kuwa wanatakiwa kujitambua kuwa wao ni watumishi wa Mungu na kazi kubwa waliyokuwa nayo ni kuhakikisha kuwa jamii inabadika.
Ameongeza kuwa kwa sasa kazi zake hizo anatarajia kuzifanyia uzinduzi baadaye mwaka huu ili kutambulisha huduma hiyo kwa jamii anayoitumikia.

Newer Post Older Post

2 Responses to “Ayubu John; Dereva wa gari anayeendesha maisha kwa nyimbo za Injili”

Anonymous said...

Na hapo ndipo shida inapoanzia. WENGI wa waimbaji wanatafuta ajira na SI kumtumikia Mungu. Ukienda kwenye show zingine za hizi nyimbo utashangaa kuona mambo yanayofanyika. Wengine wanahonga watangazaji ili nyimbo zao zipigwe redioni wapate umaarufu. Wengine wanakwenda hata kwa waganga wa kienyeji. Wengine hawaimbi mpaka walipwe pesa kwanza tena pesa hasa si mchezo. Kumwimbia Mungu unadai ulipwe kwanza? Kweli? Ukristo ni dini iliyopoteza mwelekeo!

Uisilamu ni dini inayokua kwa haraka sana kwa sababu watu wanavutiwa na misingi imara ya dini hiyo. Huko hakuna lelemama. Kama neno limekatazwa katika Kurani basi kamwe halitakubaliwa. Lakini Ukristo --- kila kitu ni sawa. Hata ukitaka ubadilishe Biblia unavyotaka mwenyewe sawa tu. Ndiyo maana kuna versions za Biblia zingine ambazo ukisoma mpaka kichwa kinakuzunguka. Jaribu kuichezea Kurani uone.

Vurugu hizi zote kuhusu Ukristo zilitabiriwa na huu ni ushahidi kwamba tunaishi katika nyakati za mwisho. Kila mtu na ashike sana alicho nacho. Mwenye masikio na asikie!!!

Anonymous said...

Mzee vipi? Mbona comments hazitoki??? Thanks, sitatia mguu wangu hapa tena. Unafiki mtupu!!!