LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

UCHUMBA HADI NDOA


Hapana shaka msomaji wa blog hii haujambo na tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuiona tena siku ya leo. Siku za hivi karibuni wasomaji wengi wameomba niwe natoa masomo ya ndoa pamoja na uchumba hadi ndoa. Nafuhi kuwa kwa saada wa Mungu leo naanza kutoa somo hili ambalo watu wengi sana wanalipenda hasa kwa wanafunzi wa shuleni na vyuoni.(Picha hii ni kwa hisani ya blog ya spotstarehe)
Naanza kwa kusema kuwa eneo hili ndilo eneo ngumu kuliko kuliko pengine unavyofikiria. Hatua ya uchumba ndiyo huwa safari ya kuelekea kwenye hatua ya kutengeneza familia yako ama kizazi chako, hivyo unahitajika umakini mkubwa katika kipindi hiki.
Pengine tuanze na kueleza maana ya neno uchumba. Uchumba ni hatua ya kijana/mwanaume kuposa ama msichana/mwanamke kuposwa. Kwa namna moja ama nyingine naweza kusema kuwa, uchumba unaanzia pale msichana anapomtambulisha mchumba wake kwa wazazi au mwanaume anapomvisha msichana pete ya uchumba au vyote kwa pamoja.
Safari ya uchumba huanza mara moja mara baada ya jinsia mbili zikikutana hapa namaanisha wakikutana msichana na mvulana ama mwanaume na mwanamke. Na mara nyingi wahusika huanza kwa kuitana kaka na dada huku ndani ya nafsi zao kukiwa na kitu cha ziada.
Baada ya kupita katika hali hiyo kinachofuata ni suala la matamanio yanaanza hasa kwa mwanaume. Hutamani kukutana na binti huyo ili amweleze juu ya hisia zake, na mara nyingi huanzia mbali ili kukwepa mwanamke asije akashtuka na kumtosa kwa madai ya kuomuona kama hajaokoka ama si mtu mwema.
Mwanaume/mwanamke huanza kufanya mambo ambayo yatamfanya mlengwa kuwa karibu naye kwa kutoa lugha nzuri ambayo siku atakapoingiza hitaji lake iwe rahisi kukubalika tofauti na kuanza kwa kukurupuka.
Kipindi hiki ndiyo huwa ni kigumu na kinaweza kuleta majuto yenye uchungu mzito maishani mwa mlengwa kutokana na kile ambacho hakutarajia kama kingetokea katika siku za usoni.
Ndoa nyingi zimejikuta zikiingia katika majuto yasiyo na kikomo kutokana na kukosea katika suala la uchumba. Baadhi ya wachumba hujikuta wanaingia katika uchumba kutokana na matamanio ya mwili. Mwanamke/mwanaume anaweza kumpenda mwanzake kutokana na uzuri wa sura wakati mwingine tabia nzuri aliyonayo bila kumruhusu Roho Mtakatifu kumwonyesha aliyewake.
Nawengi wameingia katika uchumba usio na makusudi ya Mungu kutokana na msukumo wa kuoa ama kuolewa. Kutokana na hali hiyo, wahusika wamejikuta wakiwa katika ndoa za majuto na leo hii wanatamani kuachika.

Somo hili litaendea…. Toa maoni yako kuhusiana na somo hili.

Newer Post Older Post

One Response to “UCHUMBA HADI NDOA”

Anonymous said...

Mimi ni kijana, nina mchumba ambaye nimemtambulisha kwa wazazi,lakini kulingana na mipango yetu bado hatujaipeleka kanisani lakini ilikuwa siku moja tulimkosea Mungu kwa kukutana kimwili. kitu hicho kinatutesa sana, na tumetambua na kuapa kutorudia tena na kuishi maisha matakatifu hadi ndoa kwa usalama wa roho zetu. naomba ushauri wako. David