Frola Mbasha: Nilianza kuona aibu kucheza ngoma za asili nilipofika darasa la saba, pia walikuwa wananiita mama Asha sababu ya kupenda midoli
Frola pia amebahatika kuwa na kibali katika jamii kutokana na ujumbe wa nyimbo zake kuwa na mguso wa aina yake kwa kila anayefanikiwa kuzisikiliza ama kuziona kwa njia ya video. (Pichani kushoto ni Flora Mbasha enzi ya utoto wake aliyeshika daftari)
TGM iliamua kuchoma mafuta mpaka anakoishi Frola na Tabata jijini Dar es Salaam na nilipofika mambo yalikuwa hivi.
TGM: Hodi hapa nyumbani.
FLORA: Karibu, nani mwenzangu.
TGM: Toka nje, wewe utanijuaje kama utakuwa ndani.
FROLA: Siunajua tena jiji hili limeshachafuka, unaweza ukatoka kichwa kichwa ukakutana na vibaka.
TGM: Hapana uwe na amani kabisa hii ni SIDE B leo imeamua kuja kukutembelea.
FLORA: Aman, karibu sana mdau.
TGM: Nashukuru. Bwana Yesu asifiwe
FLORA: Amen, za uzima.
TGM: Nzuri, Mungu ananisaidia.
FLORA: Haya nakusikiliza kwa maana nyingi mkionekana kwa mtu ni lazima kuwe na jambo. Nikijaribu kuangalia kila eneo naona niko salama sina sikendo hata kidogo na sitaki hali hiyo initokee maishani mwangu.
TGM: Wala usihofu mimi nimekuja kwa mema tu. Tatizo lenu wasanii ni hilo , mkiona waandishi tu mnafikiria masuala ya skendo.
FLORA: Nikweli, japo mimi huwa sifikirii sana ishu kama hivyo kwa sababu Mungu ananisaidia nisifanye mambo yaliyokinyume na mapenzi yake.
TGM: Ok. Twende kwenye pointi, nimekuja kwako kutaka kujua maisha yako kwa ujumla pamoja na huduma yako.(Pichani kulia Flora akiwa na watoto wenzake)
FLORA: Kwanza kabisa mimi nilizaliwa tarehe 1 Juni 1983 katika hospitali ya Hindu Mandhal mjini Mwanza. Baba yangu anaitwa Henry Joseph Mayalah ambaye kwa sasa ni marehemu. Mama yangu anaitwa Calorin Moses Kulola. Katika familia yetu tumezaliwa watoto wa 5, wa kiume ni mmoja aitwaye Benjamini na wakike tupo wa nne, mimi nikiwa wa pili kuzaliwa, akafuata Dorcus, Suzan na wa Mwisho akiwa ni Esther.
TGM: Tanzania ni nchi yenye amani. Watu huulizana makabila ili wapate kutaniana vizuri kwa lengo la kudumisha undugu. Niambie wewe ni kabila gani?
FLORA: Sisi ni Wasukuma wa Sengerema wilaya ambayo imo ndani ya mkoa wa Mwanza. Nimekulia katika maadili ya dini ya Kikristo, babu yangu akiwa ni Askofu mkuu wa kanisa la Evangelistic Assembilies of God. Babu na bibi yangu mpenzi Elizabeth ndiyo walionilea kwa pamoja wakishirikiana na mama yangu mpendwa.
TGM: Huduma ya uimbaji uliianza lini.
FLORA: Nilianza kuimba nikiwa darasa la tatu. Wakati huo nilikuwa nikienda na mama zangu wadogo kwenye kwaya hadi nilipokuwa na umri wa miaka kumi na tatu na ndipo nilipoanza rasmi kuimba kwaya ya kanisani na kuimbisha baadhi ya nyimbo.
TGM: Inamaana mumeo Emmanuel Mbasha alikuoa ukiwa mwimbaji wa kwaya ama ulikuwa unaimba peke yako?
FLORA: Alinioa nikiwa naimba katika Word Alive Band na baada ya kufunga ndoa Septemba 22 2002 mwaka 2002 tulianza kuimba pamoja na mume wangu tukiwa. Mungu alitusaidia mwaka 2003 nikajifungua binti mrembo aitwae Elizabeth , jambo hili hunifanya nimshukuru Mungu kwa kutupa mtoto huyo. Mwaka wa 2004 nilifanikiwa kurekodi album yangu ya kwanza niliyoita "JIPE MOYO" ikiwa na nyimbo 10.
TGM: Nikitu gani ambacho ulikipenda sana kipindi cha utoto wako.
FLORA: Nilipenda sana kusikiliza nyimbo za dini kutokana na familia yetu kuwa katika mazingira ya kidini zaidi. Pamoja na hayo nilikuwa nafuatilia kwa ukaribu sana nyimbo za Maria Kelly na Celine Dion. Vibao vya akina dada hao vilikuwa vinaukosha moyo wangu na kunifanya niwe na kazi ya kuzirekodi nyimbo zako kisha kujizimba kwa kwa sauti ya juu kama wao.
TGM: Nyimbo hizo ni za kidunia, na wewe ulikuwa katika maadili ya dini ya kikristo, hukuona kama ulikuwa unafanya makosa kufanya hivyo?(Kulia Flora akiwa na Christina Shusho jinsi alivyo sasa).
FLORA: Hapana kipindi hicho nilikuwa sielewi kama nilikuwa nafanya makosa bali nilikuwa najifunza hasa sauti zao. Kutokana na kuvutiwa na uimbaji wao nililazimika kununua daftari na kuziandika nyimbo hizo na kuzikariri mpaka nikazifahamu zote. Baada ya kuzikariri nikawa na kazi ya kuziimba hasa nyakati za usiku nilikuwa silali mapema kwa sababu ya kuimba nyimbo zao.
TGM: Ok, baada ya kuzikariri na kuziimba nyimbo hizo uliambulia nini katika maisha yako.
FLORA: Kicheko kidogo. Unajua wasanii hao naweza kusema ndiyo walimu wangu wa sauti kwa sababu kipindi hicho nilikuwa naimba wimbo kwa ‘kii’ ya juu ambayo waimbaji wengi inawashinda, na ndiyo maana mpaka leo hii nyimbo zangu huwa naziimba kwa sauti ya juu sana na kisha nashusha. Na mimi sijaenda kusomea masuala ya muziki na kupata zoezi la kuimba kwa ‘kii’ ya juu.
TGM: Mbali na kupenda nyimbo za wasanii hao kutoka ‘mamtoni’ ni mchezo gani mwingine ambao ulikuwa unapenda kuucheza enzi za utoto wako.
FLORA: Duh! Jamani maswali hayaishi tu? Any way, hakuna mchezo ambao nilikuwa naupenda sana kama ngoma za asili hasa nilipokuwa shuleni. Kila niliposikia kuna maandalizi ya tamasha, kongamano ama umitashumita nilijawa na furaha moyoni mwangu na nilikuwa nafanya mazoezi kwa kujituma kiasi kwamba walimu na wanafunzi wenzangu walinipenda.
TGM: Mlikuwa mnacheza ngoma gani?
FLORA: Tulikuwa tunacheza ngoma za makabila mbalimbali na wakati mwingine tulikuwa tunavaa nguo fupi na baadhi ya maungo yalikuwa wazi. Lakini nilipofika darasa la saba nilianza kuona aibu kucheza nimevaa hivyo mbele za watu na ndiyo ulikuwa mwisho wangu wa kucheza ngoma za asili.
TGM: Ulijiona umekua ama?
FLORA: Ndiyo. Kicheko, si unajua tena masuala ya kiutu uzima yakianza kumuingia mtu, baadhi ya mambo aliyokuwa anayafanya bila kuona aibu anaanza kufanya hivyo.
TGM: Najua kila mtoto huwa anapitia kwenye hatua ya kuigiza kama baba na mama, wakati mwingine kujipikisha ugali, wali wa mchanga kwa imani kabisa kuwa ni chakula safi na kazi nyingine nyingi. Jew ewe unakumbuka mchezo gani ambao leo hii ukiukumbuka huwa unacheka pekeyako kutokana na ulivyokuwa unaigiza?
FLORA: Kicho kidogo. Unajua wakati mwingine ukiyafikiria maisha ya utoto utabaini yanaraha sana . Mimi nilipenda sana kuigiza nikiwa mzazi na nilifanikiwa kumpeda mdoli ambao niliuita Asha. Watoto wenzangu walikazoea kuniita Mama Asha. Jina hilo lilizoeleka shuleni na hata nyumbani, jina la Frola baadhi yao walilisahau.
TGM: Mbali na kupenda sana doli, ni mchezo gani mwingine ambao ulikuwa unakufahisha ulipokuwa unakutana na watoto wenzako.
FLORA: Nilipenda sana kucheza mchezo wa lede kwa sababu nilikuwa mwepesi wa kuruka.
TGM: Nasikia enzi za utoto wako wako ulikuwa mtundu sana kiasi kwamba wazazi wako wakawa wanakuchapa viboko mara kwa mara.
FLORA: Mh! Nikweli lakini haikuwa sana kama unavyofikiri, naamini suala la mtoto kuchapwa na wazazi wake hilo huwa halikwepeki. Lakini Namshukuru Mungu muda mwingi nilikuwa nafanya vitu ambavyo wazazi wangu walikuwa wanavikubali.
TGM: Nijambo gani ambalo ulilifanya utoto na kipindi hiki ukilikumbuka huwa unajishangaa kama ni wewe uliyekuwa unafanya hivyo?
FLORA: (Kicheo kidogo). Ni suala la kuitwa mama Asha, muda wote huo nilikuwa najiona kama tayari nimesha zaa. Hiyo ilitokana na kuupenda sana mdoli wangu ambao nilikuwa nalazimika kulala nao kitandani, na wazazi wangu walipokuwa wakininyanganya nilikuwa nalia kweli mpaka wananionea huruma na wananirudishia.
TGM: Nikitu gani ambacho ulikuwa unakiogopa sana utotoni mwako? Nilikuwa naogopa kuchwa fimbo na wazazi wangu, mara nyingi nilikuwa najitahidi kufanya kwa makini kila nililokuwa naaelekezwa ilimradi tu nisitandikwe bakora.
TGM: Unakumbuka kwa mara ya mwisho kuchapwa fimbo na wazazi wako ilikuwa mwaka gani.
FLORA: Mh! Kwakweli sikumbuki hata kidogo.
TGM: Nikitu gani ambacho ulikuwa unapenda kukifanya ukubwani kama ulivyo sasa?
FLORA: Nilipenda sana niwe injinia wa kopyuta na umeme, japo ndoto hii haijatimia lakini naamini ipo siku nitapiga kitabu kwa lengo la kuyafikia malengo yangu.
TGM: Wakati tunamalizia mazungumzo yetu kuhusiana na masuala ya maisha yako ya utotoni, hebu sasa tuangalie ya sasa. Wewe ni muimbaji uliyefanikiwa kupata jina ndani na nje ya nchi. Kwa nini umeanza kupoteza mashabiki wako kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.
FLORA: Siyo kweli mimi bado ninamashabiki kibao, ila kuna baadhi ya watu wamekuwa wakidai kwamba hawanielewi kutokana na nyimbo zangu za sasa.
TGM: Kivipi tena.(Kushoto Frola akiwa na kundi laki akiwa katika kumtukuza Mungu, katikati ni mumewe Emmanuel Mbasha)
FLORA: Kuna baadhi ya watu wanadai kutonielewa kwa sababu wakati mwingine nimekuwa najichanganya na wanamuziki wa kimataifa na hasa niliposhiriki tamasha la ‘Zinduka’ hivi karibuni.
TGM: Lakini si nikweli? Iweje wewe unaimbaji muziki wa injili kisha unapanda jukwaa moja wana wasanii wa muziki wa kidunia?
FLORA: Mimi kuwa muimbaji wa nyimbo za Injili, hakunizuii kushiriki katika matamasha yenye lengo la kulitetea taifa hasa kweny kampeni hiyo ya kupambana na ugonjwa wa malaria.
TGM: Mbali na uimbaji wa muziki wa injili, kazi gani nyingine unayofanya?
FLORA: Aslimia 90 natgemea muzuki na wala sina kazi yoyoye zaidi ya kufuga kuku wa nyama.
TGM: Nakushukuru sana kwa ushirikiano wako kwangu, nakutakia huduma njema.
FLORA: Karibu tena siku nyingi.
Post a Comment