LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

Maji ya uponyaji yazua utata nchini


Mtafaruku mkubwa umeibuka katika makanisa mbalimbali nchini kuhusu uhalali wa utumiaji wa maji ya uponyaji (Anointed Water) ambayo yamekuwa yakiingizwa kwa kasi kubwa na watumishi wa kiroho kwa ajili ya kuwahudumia kondoo wao wenye matatizo mbalimbali.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, mtafaruku wa maji hayo unatokana na baadhi ya wachungaji huwatoza fedha kidogo  kondoo wao kwa madai ya kuwa wanachangia gharama za kuyasafirisha kutoka Israel ama Nigeria.
Upekuzi huo umebaini kuwa, kwa miaka ya hivi karibuni, maji mengi yanatolewa bure na mtumishi wa Mungu, Nabii Temitope Balogun Joshua a.k.a TB. Joshua ambaye ni mwangalizi wa The Synagogue Church of All Nations (SCOAN) nchini Nigeria.
Hivi karubuni, mchungaji mmoja alitua nchini akiwa na maji hayo kutoka kwa TB Joshua na kuanza kuwauzia waumini wake kwa lugha ya kuchagia kidogo gharama za usafirishaji kutoka Nigeria hali ambayo imetafasiriwa na watu wengine kwamba si sahihi.
Mbali na kuwatoza fedha kidogo waumini wake, mchungaji huyo inasemekana ameleta maji ya Kichina (feki) kutokana na kukosa nembo  ya TB Joshua ambaye kanisa lake hujaza watu wazito kutoka nchi mbalimbali.
“Maji ya uponyaji yaliyoingizwa nchini na mchungaji (anamta jina) ni feki kwa sababu hayana hata picha za Nabii TB Joshua, na amekuwa akiwapulizia waumini wake kwa kuwatoza kiasi kidogo cha fedha kwa kutumia lugha ya kuchangia gharama aliyotumia kuyasafirishia kutoka Nigeria wakati yeye alipewa bure,” alisema mchungaji wa kanisa moja lililopo jijini Dar es Salaam.
Kama kawaida yetu baada ya kupata nyeti hizo, gazeti hili lilimsaka kwa udi na uvumba mchungaji anayetumia maji hayo kujitajirisha kiana kupitia huduma hiyo na lilipompata kisha kumuwekea tuhuma zake mezani, aliruka futi mia kwa maelezo kwamba madai hayo si ya kweli.
 “Siyo kweli kwamba maji haya ni feki kama inavyodaiwa na baadhi wa wachungaji wenzangu, wakati nayachukua kutoka kwa TB Joshua niliacha kuna mengine yanatengenezwa na yametoka hivi karibuni, kwa mantiki hiyo kusema haya ni ya Kichina wanakosea.
“Kuhusu suala ya kuwatoza fedha waumini wangu na watu ninao wahudumia hili nalo si kweli, isipokuwa huwa wanachangia kiasi kidogo cha pesa kama kurudisha gharama ya pesa nilizotumia wakati wa kuzisafirisha,” alisema mchungaji huyo mwenye mwili mnene kidogo na kijipara cha mbali.
Mchungaji huyo aliongeza kuwa ili kuthibitisha kuwa maji hayo si feki tayari ameshaongea na TB Joshua kuja nchini kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa maji hayo na kukata kilimi cha watu wanaompakazia maneno ya kizushi yenye lengo la kuua huduma yake ambayo ameihangaikia kwa muda mrefu.
Wakati mchungaji huyo akipangua tuhuma hizo, kuna baadhi ya watumishi wa Mungu ambao wamekuwa wakipinga huduma hiyo ya maji na kusema kuwa, kufanya hivyo ni sawa na kuyaabudu.
Mmoja wa watumishi hao ambaye amekuwa mstari wa mbele kupinga huduma za wenzake hasa wanaotumia maji, vitambaa, fungo za gari, sabuni na nguo kuwaombea waumini alisema kuwa, leo hii Watanzania wamekuwa kama vile wamerongwa kwani wamekuwa wanaangalia ni kanisa lipi linatenda miujiza na kukimbilia.
Mchungaji huyo mwenye sifa za kutumia muda mwingi kuhubiri habari za kuponda huduma za wenzake alisema kuwa Watanzania wasipojihadhari na mlipuko wa miujiza unaofanywa na watumishi wenzake watajikuta mwisho wa siku wanaangukia motoni.  




Newer Post Older Post

One Response to “Maji ya uponyaji yazua utata nchini”

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Hayo maji ya uponyaji pamoja na vitambaa vya mkononi vilivyobarikiwa ni biashara kubwa sana hapa Marekani. Sikujua kama mambo haya yamefika nyumbani pia.

Tena hapa wachungaji wengine wanakwambia utoe dola 1,000 moja kwa moja na wanakuhakikishia kwamba ni lazima utaona muujiza angalau mmoja.

Inavyoonekana wengi wao wanafanya vizuri kwani ni matajiri wa kutupwa wakiwa na ndege zao wenyewe na wanaishi maisha ya kifahari kweli. Juzijuzi hapa wabunge kadhaa walianza kuwakoromea baadhi ya wahubiri hawa baada ya kushangazwa na matumizi yao ya kitajiri ya pesa (mmoja alinunua kikalio cha choo cha nyumbani kwake kwa dola 15,000) wakati makanisa huwa hayatozwi kodi.

Kila mmoja na ashike sana alichonacho....

(Sijui kama comment yangu hii itatoka. Nabahatisha tu!!!)