LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

ERIC SHIGONGO ATOA WARAKA WA UCHAGUZI

Ndugu zangu,
Watanzania wenzangu,
Tumsifu Yesu Kristo,
Bwana Yesu asifiwe,
Asalam Aleykhum,

Katiba yetu ya Jamhuri ya Tanzania inatutaka kila baada ya miaka mitano tufanye uchaguzi wa viongozi wetu watakaotuongoza kwenda kwenye nchi ya ahadi kwa miaka mitano, tangu uhuru wetu tumekuwa tukilifanya jambo hili na kujipatia viongozi  ambao  hakika wametufikisha hapa tulipo.

Kwa mara nyingine tena  jambo hili  linatokea kesho kutwa (Jumapili),  Watanzania  tunashiriki katika zoezi hili la kuchagua Rais na Wabunge wetu watakaotuongoza kwa miaka mitano ijayo. Nyote mtakubaliana nami kuwa   katika historia ya nchi yetu hapajapata kuwepo na uchaguzi wenye ushindani na changamoto kali  kama ilivyotokea katika uchaguzi huu wa mwaka 2010, tangu katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM)   tumeshuhudia ushindani mkali  kati ya wagombea  kuliko  uchaguzi mwingine wowote uliowahi  kufanyika nchini mwetu. Hili ni jambo la kujivunia.

Keshokutwa ni  siku muhimu sana katika maisha yetu, siku  ambayo  tutafanya  maamuzi  juu ya  maisha yetu ya baadaye  kwetu sisi na watoto wetu ambao hawatashiriki kupiga kura,  hii ina maana tumebeba  dhamana kubwa sana ya watoto  na wajukuu zetu pia, keshokutwa ndio siku ambayo sisi Wananchi wa kawaida tutaonyesha uwezo wetu kwamba  ndio waajiri wa viongozi wetu. Hakika  hii ni siku muhimu sana.
Nimeamua kuandika waraka huu kwa lengo la kuwakumbusha  jambo moja kwamba, kwa miaka 49 tangu tupate uhuru, nchi yetu imefaidi amani na utulivu ambao majirani zetu wengi hawana. Amani ni kitu adimu sana nchini Kenya, Uganda, Burundi,  Sudan na kwingineko,  walifanya makosa  yaliyofanya  Njiwa wa Amani  akaruka na kuondoka zake!

 Ndugu zangu,  Watanzania wenzangu,
Ni vyema kukumbuka kuwa, katika maamuzi yetu ya keshokutwa, kosa dogo   tu linaweza kufanya amani ya nchi hii kuwa historia, jambo ambalo  binafsi sitaki kulishuhudia kwa macho yangu na hata vizazi vijavyo sitaki vije kunihukumu kuwa nilishindwa kuitunza Amani.  Hakuna anayewaza kwamba  kama hatutafanya maamuzi sahihi keshokutwa, tuna masaa machache  kabla historia ya nchi yetu haijabadilika kwani hata katika nchi  zisizo na amani walianza hivi hivi na hakuna aliyekuwa na taarifa kwamba wangeishia kwenye kambi za wakimbizi.

Watanzania wenzangu,
Nchi  yetu imepita katika vipindi vigumu vingi;  wakati wa kupigania uhuru wa nchi yetu kutoka kwa Wakoloni, Azimio la Arusha, Operesheni Vijiji, Vita vya Kagera, kuzama kwa MV Bukoba, uchaguzi  wa mwaka 2005 n.k.,   lakini katika vipindi vyote hivi  tulisimama pamoja kama nchi,   kuhakikisha tunazishinda changamoto  hizo tukiwa familia moja ya Watanzania. Ndugu zangu hii ndiyo historia yetu kama Watanzania, ya  kupanda pamoja na kushuka pamoja. Kulia pamoja na kufurahia pamoja.

Kwa mara nyingine tena  ndugu zangu, keshokutwa  asubuhi Busara,  Hekima na Uvumilivu wetu  unawekwa kwenye mzani ili upimwe, ndio maana naandika waraka  huu kabla ya siku ya kesho  kuwaasa tuifikirie Tanzania yetu,  tuwafikirie watoto wetu,  tuwafikirie wajukuu zetu na  kujiepusha na  maamuzi mabaya yatakayotokana na chuki,  jazba na hasira na kuchukua uamuzi utakaokuwa na faida kwetu na vizazi  vitavyokuja baada ya sisi.

Kuna vyama vilivyosimamisha wagombea wa Urais na Wabunge, kipo Chama Cha Mapinduzi, CHADEMA, CUF, UDP, TLP, NCCR-Mageuzi, APPT Maendeleo, NLD, Demokrasia Makini, CHAUSTA, UMD, SAU, NRA, AFP, UPDP, JAHAZI Asilia na TADEA.  Kati ya vyama vyote hivi hakuna hata kimoja cha kukipuuza, hakuna anayeweza kudai  Chama  fulani ni bora kuliko kingine,  wenye uamuzi huo ni wananchi wa Tanzania hiyo  siku ya keshokutwa.

Vyote ni vyama,  kila kimoja  kinataka  kiwe kinara  katika safari yetu kuelekea katika nchi ya ahadi na vyote vina wafuasi waliotapakaa nchi nzima na watapiga  kura siku ya keshokutwa. Hii ina  maana kwa sababu  ya tofauti za Kiitikadi,  Watanzania   tumegawanyika katika makundi,  wapo CCM, wapo TLP, wapo CUF n.k.
Ndugu zangu,
Pamoja na tofauti zetu hizi,  bado tunaunganishwa na kitu kimoja kikubwa ambacho ni Utanzania wetu,  mwisho wa siku sisi ni Watanzania watoto wa baba mmoja atiwaye Tanzania  na tunafanana katika jambo moja;  HATIMA! Hatima yetu ni moja,  hakuna anayeweza kukataa  ukweli kwamba  sote tunahitaji huduma bora za afya,  elimu bora kwa watoto wetu, barabara, maji, ajira na  nafasi sawa ya kuendelea mbele kimaisha. Usawa wetu huu,  ndio unatufanya tuweke pembeni tofauti zetu zote na kufanya maamuzi sahihi  siku ya kesho.  
Kila mmoja wetu anayo haki ya kumchagua kiongozi yeyote anayempenda bila kushinikizwa, hii ni haki ya Kikatiba.  Waraka huu hauna lengo la kumshawishi mtu yeyote  achague Chama fulani na akiache kingine,  bali  ni   kukumbusha Utanzania na Amani yetu, mambo  mawili makubwa ambayo hakika hatuhitaji kuyapoteza  kwa  gharama  yoyote  kwani  kuyarejesha ni  kazi ngumu  ambayo inaweza hata kugharimu maisha yetu.

 Nayasema haya sababu mengi yameongewa  na Wanasiasa wakati wa kampeni kwa lengo la kutushawishi  tuwaunge  mkono,  tumeshuhudia hata vifo vya watu sababu ya Siasa!  Jambo ambalo hakuna mtu aliyetegemea wakati kampeni zinaanza.

Wapo waliohubiri chuki za kidini majukwaani  na hata  madhabahuni,  wapo waliohubiri Ukabila, rangi na kadhalika ili tu wajipatie  wafuasi  bila kufahamu kuwa hiyo ni mbegu mbaya ambayo  kabla  ama baada ya uchaguzi inaweza kuliteketeza  Taifa letu na kutuacha baadhi yetu  makaburini  na Amani  ambayo kwa kipindi kirefu tumejivunia ikiwa imepotea.  Viongozi wa aina hii  siku ya keshokutwa hata kama ni wataalam kiasi gani wa kuongea majukwaani,  inabidi  wanyimwe kura.

Katika kitabu cha Paulo Coelho, kiitwacho The Alchemist, anaongelewa mchungaji mmoja kijana aitwaye Santiago, ambaye ndoto yake ilikuwa ni kusafiri  dunia nzima ambapo aliacha masomo ya Upadri ili  awe mchunga Kondoo na kutimiza lengo lake.  Katika safari yake aliswaga  kundi la Kondoo  kuelekea katika nchi ya Andalusia.

Aliwapeleka kondoo alikotaka yeye na  kuwafanya  wafanye alivyotaka, kama alitaka wanywe maji aliwapeleka bwawani na kama alitaka wale nyasi aliwapeleka malishoni. Siku moja  Santiago alisimama na kuwaangalia  kondoo wake kwa huruma moyoni mwake akasema: “Hawajui niwapelekako, nikiamua kuwachinja mmoja baada ya mwingine hakuna atakayeshtuka wala kukimbia, kwani hawa ni Kondoo,  wa mwisho atajikuta ameshabaki peke yake lakini bado hatakimbia.”

Ndugu zangu,
Siku ya keshokutwa tuna kazi kubwa ya  kuchagua wachungaji  watakotuchunga  kwa miaka mitano, hivyo ni lazima tunahakikisha tunachagua mchungaji ambaye hatatutelekeza kama kondoo wa Santiago, tukatae kufanywa Kondoo bali   tufanye maamuzi yenye faida kwetu, badala ya kupelekwa au kuhamasishwa na jazba tunazopandikizwa.

Tukumbuke sisi ndio nguvu ya taifa hili, lazima tuwakatalie watu wote wanaotaka kutugawa na kuiingiza nchi yetu katika  matatizo eti kwa sababu tu wanataka  kwenda Ikulu. Tusiwe kondoo bali tuwe na uwezo wa kuchanganua kila sentensi inayotoka  midomoni mwa  Wanasiasa,  tukikumbuka  msemo  usemao “Nyuma ya sentensi ya mwanasiasa kuna sentensi nyingine.”  Wanasiasa walio wengi huwa hawamaanishi wanachokisema, siku zote wana moja kichwani.

Hivyo ni vizuri  kuachana na  sentensi  za  mbele  na kwenda nyuma  ya sentensi hizo, huko ndiko  tutaukuta ukweli kuwa   lengo halikuwa kusomesha watu bure au kuondoa kodi,  au  kutimiza ahadi zote zinazotolewa bali  ni Ikulu vichwani mwao! Kwa akili alizotupatia  Muumba  wetu ni lazima tuwe na uwezo wa kupambanua  kila jambo  na kufanya uamuzi sahihi siku ya kesho.

Uamuzi wowote utakaofanya,  usiwe wa ushabiki tu bali utakaotuwezesha  kusonga mbele kama nchi moja, watu wamoja na  baada ya uchaguzi,  sote tukubaliane na matokeo  kama CCM watakuwa wameshindwa wawe tayari kuwaachia Wapinzani ili haki itendeke  na kama  Chadema au CUF au TLP watakuwa wameshindwa  kwa haki asiwepo mtu yeyote wa  kukataa matokeo na kutushauri   sisi Watanzania tuingie mitaani na  kufanya vurugu ambazo mwisho wa siku zitaiondoa Amani yetu.

Najua vijana wengi wamejazwa jazba kwamba kama matokeo hayatakuwa  kama walivyotaka wao basi damu itamwagika, lakini niseme jambo moja kwamba ni  mtu mjinga tu anaweza kukubaliana na jambo hili na kutumiwa kama ngazi na Wanasiasa na hatimaye kutesa ndugu zake. Ukishindwa kubali, baada ya hapo tuungane kujenga Majimbo na nchi yetu.

Ndugu zangu,
Hakuna kitu kibaya kama kupoteza amani,  angalieni majirani zetu wanavyoihangaikia! Ni vizuri sana kujifunza kutoka kwao kabla sisi hatujafikiria kujiingiza katika vurugu sababu ya wanasiasa ambao siku zote wapo tayari kuingia Ikulu  hata kama gharama ni damu yetu! Hii sio sahihi hata kidogo, lazima tuzikatae kauli hizi kutoka kwa wanasiasa na keshokutwa  tufanye maamuzi sahihi yenye manufaa kwa nchi yetu.

Chama tawala (CCM)  kimejieleza  kupitia kwa Mgombea wake,  Dk. Jakaya Mrisho Kikwete  kimejinadi  kwamba  pamoja na  matatizo yanayosababishwa na umasikini, kimejitahidi   kadri ya uwezo wake kujenga Uchumi wetu.   Vyama vya Upinzani  navyo  viliendelea kudai hakuna kilichofanywa na CCM  tangu Uhuru wetu,  yote ni mabaya! Yote ni sifuri! Sana sana ni  ufisadi peke yake!  Hivyo wachaguliwe wao ambao wataboresha maisha ya  Watanzania.

Wakati mwingine tumesikia hata Matusi katika majukwaa ya Kisiasa zote hizi ni  kampeni lengo  ni kuitafuta  kura yangu na yako. Ndugu yangu,   sitaki kukushawishi keshokutwa umchague fulani, ila nasema  tumia akili yako kama mzani  ili upime  kauli za Wanasiasa na kuona kama tunakwenda mbele au tunarudi nyuma kama nchi,  Mgombea  mwongo yeyote hastahili kupewa kura yako.

Nchi yetu iko njia panda,  inahitaji  viongozi  imara  wanaoweza kuchagua  kwenda kulia ama kushoto si kubaki katikati,  kama kweli tunahitaji  kusonga mbele. Binafsi sikubaliani na nafasi ya pili ama ya tatu katika Afrika Mashariki,  lazima siku moja Tanzania iwe namba moja.  Jambo hili linawezekana  kama  tutaweka uongozi imara madarakani.

Hata kama hali ni ngumu kiasi gani ni lazima tuchukue hatua makini kusogea mbele! Huu ni ukweli.  Najua kama Watanzania tunayo matatizo mengi  hivyo kiongozi yeyote tutakayemchagua kesho lazima awe ni yule atakayetuhakikishia  kwamba atashughulikia matatizo yetu  si tu  hotuba nzuri jukwaani na jazba nyingi zisizo na kipimo.

 Siku ya keshokutwa ndio siku ya kufanya uamuzi huu muhimu bila kufanya makosa, tuwapime wagombea wetu kwa historia zao na mafanikio waliyotuletea katika nyanja nilizozitaja hapo juu!

Siku ya keshokutwa ni siku ambayo tunatakiwa kufanya  si tu mambo yanayoshangiliwa na wengi bali mambo ya lazima kufanya, hata kama hayatashangiliwa ili mradi yawe  na faida kwa nchi yetu. Kwa haya niliyoyasema ndugu zangu nawaomba siku ya keshokutwa  tuwe makini sana katika uamuzi tutakaofanya,  kamwe tusifuate ushabiki tu na kuwa bendera inayofuata upepo, bali tutumie akili zetu vizuri kuchagua viongozi bora watakaotuvusha kipindi cha miaka mitano kwa mafanikio. Kwa haya machache nawatakieni uchaguzi mwema siku ya kesho,  utakapoingia kwenye chumba cha kupigia kura,  ifikirie nchi yetu, fikiria wazazi wako, watoto wako, ndugu zako,  rafiki zako baada ya hapo Mungu akusaidie ufanye uamuzi sahihi.

Mungu ibariki Tanzania,
Mungu wabariki  Watanzania.
Ahsanteni.


Newer Post Older Post

One Response to “ERIC SHIGONGO ATOA WARAKA WA UCHAGUZI”

Mchukia UDAKU WA SHIGONGO said...

Najua comment hii haitatoka kwani itakufanya UFUKUZWE KAZI lakini naandika tu anyway.

Mwambie Shigongo kwamba mimi nataka ZE UTAMU irudi. Mbona alitishwa tu kidogo halafu akaiua??? Mwoga nini?

Please soma huu mjadala hapa:

http://changamotoyetu.blogspot.com/2010/09/mimi-najifunza-kitu-wewe-je.html

Kalagabaho na shigongo wako.