KABULA J GEORGE NA MUMEWE WAHITIMU MASOMO YA UCHUNGAJI NA UNABII
Picha ya chini na juu inamuonyesha George Kayala akicheza ndani ya Huduma ya Neno la Upatanisho siku ya kuhitimu masomo ya Uchungaji na Unabii, kushoto kwake ni Kabula.
Kabula akiimba kwa furaha wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika ndani ya ukumbi wa Huduma ya Neno la Upatanisho Novemba 13,2010
Baada ya kusifu zamu ya kumwabudu Mungu iliwadia, Kabula akimwabudu Mungu katika roho na kweli
George naye hakuwa nyuma katika kumwabudu Mungu siku hiyo
George na Kabula wakiwa katika picha za pozi baada ya kuhitimu masomo ya Uchungaji na Unabii Novemba 13,2010
Mwihava akicheza kwa ustadi wimbo wa Kumbuka Kushukuru ndani ya Huduma ya Neno la Upatanisho iliyopo Bustani ya Eden Kivule Jumapili iliyopita (Novemba 14,2010). Picha chini Kabula na mumewe George na rafiki yao Renata Samba wakimwabudu Mungu wakati wa ibada Jumapili ya Novemba 14,2010 ndani ya Huduma hiyo. Glory George wa katika akimsifu Mungu wakati wa ibaada
Kabula akimwabudu Mungu kwa kumanisha
George Kayala naye akionekana amezama katika kumwabudu Mungu
Dada huyo jina tunalihifadhi akiwa amelala chini baada ya kuombewa mtumishi wa Mungu Nicolaus Suguye ambaye ni mwangalizi wa Huduma ya Neno la Upatanisho hayupo pichani. Dada huyu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya damu na sasa ni mzima wa afya.
4 Responses to “KABULA J GEORGE NA MUMEWE WAHITIMU MASOMO YA UCHUNGAJI NA UNABII”
Sasa itabidi uachane na mambo ya giza ya udaku wa Shigongo. Jitoe kabisa kumtumikia Mungu....
hongereni sana kwa kupata uchungaji, ila kuna kitu kinanitatiza katika blog yako naona kwenye blog yako mambo mengi na picha nyingi zinakuhusu wewe mwenyewe na familia yako tu!!! kwa asilimia 80.Jaribu kutuwekea matukio mbalimbali ya makanisa tofauti naona ni wewe tu kama vile unajiadvertise kupita kiasi! sorry kama nitakuwa nimekukwaza labda utembelee na strictly gospel you can get some ideas so as to change.Mama Alice U.K.
UNABII UNASOMEWA???
UNABII HAUSOMEWI - SIMPLE AND CLEAR !!!
Post a Comment