Gwajima
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ametoa mpya kwa kutahadharisha kuhusu tiba ya kikombe cha Mchungaji Ambilikile Masapile wa Samunge, Loliondo kwa kusema kuwa endapo dawa hiyo anayoitoa inaponyesha watu asibughudhiwe wala asipigwe vita.
Alisema kwamba hajajua kama dawa hiyo inaponyesha watu au laa na kueleza kuwa, kama wagonjwa wanaoitumia wanapona ni jambo zuri, hivyo hakuna sababu ya kubughudhiwa bali apewe ushirikiano ili aendelee kuwasaidia wagonjwa.
“Hao watu wanaompiga vita Masapile ina maana wameshindwa kuwasaidia wagonjwa na ndiyo maana wanakimbiwa na kubakia kulalamika huku wakiponda huduma anayoitoa mchungaji huyo. Wagonjwa ni wajanja sana, wanaangalia ni wapi wanaweza kupata uponyaji,” alisema Gwajima.
Aliongeza kusema kuwa, kunywa dawa ya miti si dhambi kwani hata vidonge vinavyotumika kutibu magonjwa mbalimbali vinatokana na mimea isipokuwa huwa vinatengenezwa kiwandani, hivyo haoni tatizo kwa Masapile kutumia uponyaji wa mizizi anayodai kuoteshwa na Mungu.
2 Responses to “Gwajima”
ni suala zuri kwa mchungaji au mtumishi mmoja kutambua kazi anayofanya mtumishi mwingine hata kama ametoka kitofauti.. namuunga mkono gwajima kwani ata yesu alishaletewa kes ya namna hii kuusu wanafunzi wa yohana kufanya kazi kama za yesu yesu akawaambia "WAACHENI WAKO ASIYEKUWA KINYUME CHETU YUKO UPANDE WETU " hivyo sioni ugumu wa jambo hili kwa sbs tu masapile si mlokole

Post a Comment