|
SARAH SANGA |
Mwimbaji wa
nyimbo za injili nchini Sarah Sanga anayetesa na kibao cha Simama Baba Unitete,
amelitaka jeshi la polisi nchini kumtafuta mtu aliyevumisha uzushi kuwa, Bahati
Bukuku amefariki dunia kwa ajali wakati anatokea mkoani Mbeya.
Akizungumza
na TGM jana jijini Dar es Salaam, Sahar alisema kuwa mtu aliyeeneza taarifa hizo ni sawa na mtu yeyote anayetishia kuua na
hilo ni kosa la jinai hivyo ni vizuri akasakwa ili sheria ishike mkondo wake.
“Nalitaka jeshi
la polisi limsaka mtu aliyevumisha kifo cha Bahati kwani kimewashtua watu wengi
na hilo pia ni kosa la jinai kwani ni sawa na kwamba ametishia kuua kwa njia ya
maneno hivyo ni bora akatafutwa,” alisema Sarah.
Sarah alisema
kuwa polisi wanauwezo wa kulifanyia kazi hilo hasa kwa kuchunguza ujumbe huo wa
simu uliokuwa unasambazwa kwa njia ya simu ulianzia kwa nani na huyo ndiyo
anaweza kusema kukweli wa nani aliyevumisha tukio hilo.
Mwanzoni mwa
wiki hii kuna uvumi ulienezwa kila kona ya nchi kwa njia ya simu za mkononi na
mitandano ya kijamii kama blog na facebook kuwa Bahati Bukuku alifariki baada
ya kupata ajali mbaya wakati anatoka mkoani Mbeya.
Bahati
alipotafutwa kuzungumzia suala hilo alikiri naye kupokea habari kama hizo na
hakujua ni nani alizieneza na kudai kuwa yote anamwachia Mungu kwani yeye ndiye
anayejua mwisho wa uhai wake.
Wakati huo
huo, Saraha amewataka wadau wa muziki wa injili kujipatia nakala za albamu yake
ya Simama Baba Unitetea ambayo ameisambaza kwenye maduka mbalimbali jijini Dar
es Salaam.
“Baada ya
kutoa albamu yangu nilipokea maombi mengi ya watu wakiomba kuipata nami
nimesikia ombi langu na nimeamua kuisambaza katika maduka mbalimbali jijini Dar
es Salaam hasa Kariakoo ikiwa na nyimbo nane,” alisema Sarah.
Alizitaja
nyimbo zinazounda albamu hiyo kuwa ni Simama Baba Unitetee, Haleluya, Anajibu
Maombi, Yesu Napiga Saluti, Tanzania, Mwana wa Adamu, Moyo wa Wangu na Siku za
Mwisho.
Post a Comment