MWINJILISTI KABULA: NITAING’ARISHA MBEYA JULAI 21
MWIMBAJI wa
nyimbo za injili nchini Mwinjilisti Kabula George amesema kuwa atainga’ara
Mbeya siku ya tamasha la kuitambulisha
albamu yake ya Nitang’ara litakalofanyika katika kanisa la Moravian Usharika wa
Yerusalem Airport.
Akizungumza na
Tanzania Gospel Music leo muda mfupi uliopita, Mwinjilisti Kabula amesema kuwa
hii ni mara ya kwanza kutoa huduma katika mkoa wa Mbeya hivyo atahakikisha
anaweka historia katika fani ya muziki huo.
“Nitaing’arisha
Mbeya Julai 21 mwaka huu katika tamasha la kuitambulisha DVD yangu ya Nitang’ara
Tu. Nipo katika mazoezi makali kwa ajili ya kuwafurahisha Wanambeya watakaofika
katika shughuli hiyo.
Tamasha hilo
litanogeshwa na wakali wa muziki huo kutoka mikoa mitatu ya Tanzania Bara
wakiongozwa na Ambele Chapanyota,Christina
Shusho, Enock Jackson na wengine wengi.
Mratibu tamasha
hilo George Kayala alisema kuwa
kiingilio katika tamasha hilo kitakuwa elfu 1000 kwa wakubwa na 500 kwa watoto
ili kuwawezesha watu wengi kufika kushuhudia tamasha hilo.
“Tumeamua
kuweka kiingilio kidogo ambacho kitamuwezesha kila mmoja kuingia kushuhudia
tamasha hilo ambalo tunaamini litaweka historia mkoani hapo, kwani pia ni mara
ya kwanza kwa mwinjilisti Kabula kutoa huduma mkoani hapo,” alisema Kayala.
Tamasha hilo
linadhaminiwa na , Ushindi Redio ya Mbeya, GMK Production, RGC Miracle Center
Tabata Chang’ombe, Shalom Production, Mbeya Yetu blog, Tanzania Gospel Music
blog na The Genesis Global College.
Post a Comment