LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

Jennifer Mgendi atema cheche kwa majangiri wa sanaa



Mkongwe wa muziki wa Injili nchini Jennifer Mgendi ametema cheche kali kwa majangiri wanaojihusisha na shughuli ya kudurufu CD,VCD na DVD  na filamu za wasanii wa fani mbalimbali na kuziuza bila idhini yao huku wakiwaacha wahusika wakiambulia vijisenti vidogo kutoka kwa wasambazaji wa kazi zao, ishu kamili anatelemka nayo  Hemed Kisanda.

Akiteta na safu hii hivi karibuni, Jennifer alisema kuwa, ili kukomesha ujangiri huo, waimbaji wote wa muziki wa Injili yawapasa kushikamana na kuunda mtandao nchini nzima ambao utashughulika na kuwakamata wamachinga wanaouza kazi hizo na kwa kufanya hivyo, watafanikiwa kudhibiti wimbi hilo ambalo limewatajirisha watu wasiotoa jasho lolote zaidi ya kukaa ofisini mwao na kuanza kudurufu CD,VCD na DVD.

Jennifer anayetesa na albamu yake mpya ya Kiu ya Nafsi  alisema kuwa, yupo katika hatua za mwisho za kukamilisha  mwendelezo wa filamu ya TEKE LA MAMA (Part II) yenye mafundisho kwa ajili ya watu wa rika zote na inatarajiwa kuwa tarari mwezi Machi mwaka huu.

Mbali na Part II ya filamu ya Teke la Mama, muvi zake zingine ni pamoja na  ‘Joto la Roho’ ya mwaka 2004 na ‘Pigo la Faraja’ ya 2005, na washiriki wote waliocheza filamu ya kwanza ya Teke la Mama ndiyo watakaoendelea na nafasi zao.


Newer Post Older Post

One Response to “Jennifer Mgendi atema cheche kwa majangiri wa sanaa”

Anonymous said...

Tazama hapa:

http://nyimbozadini.blogspot.com/2010/07/ujumbe-na-angalizo-kutoka-kwa-dada.html