LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

MTUME WA UREJESHO KUUZA KITABU CHAKE LEO


Mtume Nyaga akiuza kitabu cha Nguvu ya Pesa na Utajiri na waamini wanaonekana kukichangamkia sana


Mtume wa Urejesho wa Kanisa la RGC Miracle Center Tabata Chang’ombe, Peter Nyaga leo anatarajia kuendelea kuuza kitabu chake  kiitwacho Nguvu ya Pesa na Utajiri ambayo kimefanyika msaada mkubwa katika jamii. Akizungumza na Tanzania Gospel Music muda mfupi uliopita, Mtume Nyaga amesema kuwa saa 3:00 asubuhi hii atakuwa na maombi ya unabii kwa mtu mmoja mmoja na vitabu vitapatika kwa shilingi 5000 badala ya 50,000. Mtume Nyaga amesema kuwa ndani ya kitabu hicho kuna masomo ya ujasiliamali hasa wa kutengeneza sababu, batiki nk.

Hiki ndiyo kitabu cha Nguvu ya Pesa na Utajiri cha Mtume Nyaga

KWA NINI WATU WENGI HAWAJIBIWI MAOMBI YAO? - 2

Apostle George Kayala

Namshukuru Mungu kwa kutuamsha salama tena siku ya leo kwani kuna wengi walitamani kuiona siku ya leo lakini hatuku nao. Si kwamba mimi na wewe ni watakatifu sana kiasi kwamba tuwe wazima mpaka sasa bali ni neema yake Mungu aliyotupa tena leo. Nimaombi yangu hata sasa unaposoma somo hili jitahidi kuwa katika hali ya toba wakati wote kwani hujui sekundi moja ijayo nini kitatokea katika maisha yako. Mimi na wewe hatujui ni nani anayeweza kutwaliwa siku ya leo. Tambua hakuna mtu anayejua siku yake ya kufa. Watu wengi hujua mipango yao ya maisha na kujiwekea malengo ya muda mfupi na mrefu wakiwa na uhakika wakufika huko.


Swali waliotangulia jana na usiku wa kuamkia leo ina maana hawakuwa na malengo? Jibu ni kwamba nao walikuwa na malengo kama wewe ila hawakujua siku yao ya kufa na waliamini kabisa kuwa watatimiza malengo yao. Ni maombi yangu malengo yako uyaweke mkononi mwa Bwana ili akufanikishe hata kama atakuchukua leo utakuwa na faida ya kuishi naye milele.
Ame, ngoja tuendelee na somo letu la KWA NINI WATU WENGI HAWAJIBIWI MAOMBI YAO? Jana nilimaliza kwa kusema kuwa kila unaloomba Mungu anauwezo nalo na haakuna la kumshinda. Mandiko katika kitabu cha Yeremia 32:27 yanasema “Tazama mimi ni BWANA Mungu wa wote wenye mwili  je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?.
Kumbuka kuwa Mungu ndiye ampaye kila mtu ampendaye. Swali la kujiuliza ni kweli wewe hakupendi mpaka asisikie maombi yako? Kitabu cha  Danieli 4:25, 34 maandiko yanasema kuwa; "Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu naye humpa yeye amtakaye, awaye yote . . . mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi."
Ukitaka Mungu akujibu kwa haraka maombi yako, hakikisha unapoingia kwenye maombi uwe umeshajitakasa na kusamehe wale waliokukosea. Lakini wakati mwingine wewe ndiye unayesababisha Mungu achelewe kujibu maombi yako kwa sababu unaingia kwenye maombi ukiwa katika chuki na waliokukosea.
Maandiko yanasema kuwa Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii.” Yohana 9:31. Kama utakuwa na kawaida ya kuingia katika maombi huku ukiwa na fundo la dhambi ya kutowasamehe waliokukosea na kujitakasa, hakika utaomba na kufunga mpaka unapata vidonda vya tumbo na hutapata hitaji la moyo wako.
Maandiko yanaendelea kusema kuwa Vumilianeni na kusameheana. Mtu akiwa na lalamiko lo lote dhidi ya mwenzake, sameheaneni kama vile Bwana alivyowasamehe ninyi. Zaidi ya maadili haya yote jivikeni upendo, ambao ndio unaofunga kila kitu pamoja katika amani kamilifu,” Wakolosai 3:13-14. Katika maandiko haya Mungu anatoa amri ya kumsamehe kila mmoja. Hii inamaanisha kwamba kama unataka kusamehewa dhambi zako lazima kusamehe wale ambao wamekukosea au wametenda  dhambi juu yako.
Na kama hiyo haitoshi Mungu anakutaka usamehe hata kama unakosewa mara kwa mara. Mathew 18: 21-22;  Ndipo Petro akamjia Yesu na kumwuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Je, hata mara saba?” Yesu akamjibu, ‘‘Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.’’
Kwa leo naishia hapa nakusihi endelea kufuatilia somo hilo naamini litakusaidia.
Naitwa Apostle George Kayala
Kwa maoni na ushauri niandikie kwa barua pepe; gmkproduction77@gmail.com

KAMPENI YA KOMESHA UCHAWI NA MCHAWI KUENDELEO KESHO


ILE kampeni ya Komesha Uchawi na Mchawi Lete Roho kwa Yesu inaendelea tena kesho katika huduma ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM) ikiongozwa na Nabii Nicolaus ambaye ni mwangalizi wa huduma hiyo. Akizungumza Tanzania Gospel Music muda mfupi uliopita, Nabii Nicolaus mesema kuwa, maombezi ya kesho yatawahusisha watu wenye shida mbalimbali waliofungwa na nguvu za giza na kukosa kazi na kesho itakuwa siku ya kufunguli

Nabii Nicolaus akimshika mtoto ili sauti yake isikike. Kusho ni mama wa mtoto huyo Josephine akishuhudia jinsi ya kupata muujiza wa kujifungua mwanaye wa kiume bila uchungu kuuma baada ya kutabiliwa hivyo na nabii.


Nabii Nicolaus akifurahi baada ya sauti ya mtoto kusikika


Nabii Nicolaus akiwaombea waamini Jumapili iliyopita


Mama huyu akitapika vitu alivyolishwa kichawi na alipokea ukombozi baada ya kuombewa na Nabii Nicolaus.


Bwana Masamaki kushoto akitoa ushuhuda wa kuteuliwa kuwa kamishina wa Idara forodha TRA

EUGINE KUSHUHUDIA UZINDUZI WA HESABU BARAKA



Joyce Mwaikofu
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe. Eugine Mwaiposya anatarajia kushuhudia uzinduzi wa albam ya pili ya mwimbaji wa nyimbo za  injili nchini, Joyce Mwaikofu itwayo Hesabu Baraka utakaofanyika Agosti 4 mwaka huu ndani ya kanisa la EAGT Kipunguni A Ukonga Banana barabara ya Kitunda ikiwa katika mfumo wa DVD.
Akizungumza na Tanzania Gospel Music jana jijini Dar es Salaam, Joyce alisema kuwa Mwaiposya ataungana na mbunge mwenzake wa Iramba Magharabi Mhe. Mwigulu Nchemba ambaye ndiye mgeni rasmi katika uzinduzi huo wenye  lengo la kuchangisha  fedha za kununulia vyombo vya muziki na nyingine kumalizia ujenzi wa kanisa hilo linaloongozwa na mmewe mchungaji John Mabega.
 “Mwaiposya amekubali kuungana na Nchemba katika uzinduzi wa albam yangu ya pili na nina amini kuwa uwepo wao utawezesha kupatikana kwa fedha za kununulia vyombo vya muziki ambavyo vitatumika kanisani pamoja na kumalizia ujenzi wa jengo la kanisa hilo,” alisema Joyce.
Mwimbaji huyo ambaye kitaaluma na mwanasheria wakili alisema kuwa, uzinduzi huo utanogeshwa na wakali wa nyimbo za injili ambao atawaweka hadharani wiki hii baada ya kukamilika mazungumzo kati yake na wao na amewataka mashabiki wa muziki huo kufika kwa wingi siku tukio.
“Nimeanza kuongea na waimbaji mbalimbali ambao ni wakali wa nyimbo za injili nchini na nitawaweka hadharani mapema wiki hii hivyo nawatakama mashabiki wa muziki wa injili kufika kwa wingi katika tukio hilo ili kuwezesha kupata fedha hizo ambazo zitaendeleza kazi ya Mungu,” alisema mama mchungaji.
Joyce alisema kuwa uzinduzi huo ambao hautakuwa na kiingilio utaanza saa 7:00 mchana na kumalizika saa 12:00 jioni.

KWA NINI WATU WENGI HAWAJIBIWI MAOMBI YAO?

Apostle George Kayala
Wapendwa katika Bwana, nimesukumwa moyoni kuwa natoa masomo ya biblia kwa njia hii ikiwa ni moja ya kukumbushana juu ya safari yetu ya kuelekea mbiguni. Katika somo letu la leo tutaangalia kwa nini watu wengi hasa waliookoka huwa hawajibiwi maombi yao kama wanavyoomba? Kama ni bidii ya maombi wanafanya lakini haja ya maombi yao haitekelezeki. Wakati mwingine mpaka wanafikiri kuwa Mungu hasikii maombi yao na kujikuta muda mwingi wanabaki kunung’unika. Watu wengi hawajui kuwa kushindwa kujibiwa kwa maombi yao kunatokana na jinsi wanavyoomba.
Wapo wanaoomba ili wananikiwe wapate kuwatishia wenzao, ama kutumia kinyume na mapenzi ya Mungu kile anachoomba. Unaweza kukuta mtu anasema mimi naomba Mungu anipe pesa kwa ajili ya huduma yake lakini kumbe moyoni mipango iko tofauti.
Kaka wewe ni miongoni mwa watu ambao wameomba muda mrefu bika kupata haja ya kile unachoomba soka kitabu hiki. Yakobo 4:3 “Hata mwaomba walahampati kwa sababu mwaomba vibaya ili mvitumie kwa tamaa zenu”.
Ili Mungu akujibu kile unachoomba inakupasa kuomba sawasawa na mapenzi yake na siyo yako. Kumbu kuwa Mungu ni Roho, hivyo huwezi kumdanganya kwa lolote katika maombi yako ambayo naweza kuyaita ni ya ubabaishaji.
Katika kitabu cha 1Yohana 5:14-15 biblia inasema Na huu ndio ujasiri tulionao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 15 Na tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba .
Naamini mpaka hapo utakuwa umejifunza kitu fulani kwa haya machache niliyokweleza. Nitaendelea na somo hili kesho naomba usikose kulifuatilia kwani ni imani yangu mpaka mwisho wa somo utakuwa umejifunza kitu na utabadili mwenendo wa maombi yako.
Elewa kuwa kila unaloomba Mungu anauwezo nalo na haakuna la kumshinda. Mandiko katika kitabu cha Yeremia 32:27 yanasema “Tazama mimi ni BWANA Mungu wa wote wenye mwili  je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?.Sikiliza msomaji mpendwa Hakuna jambo gumu la Kumshinda Bwana.

Naitwa Apostle George Kayala
Kwa maoni na ushauri niandikie kwa barua pepe gmkproduction77@gmail.com

SAUTI ZA SIFA WA HUDUMA YA WRM WAKICHEMKA MADHABAHUNI


Hawa ndiyo Sauti za Sifa wakimtukuza Mungu

Sauti za Sifa wakiwaongoza waamini waliofika WRM leo kumsifu Mungu wa kweli.


Kitendo hiki cha muziki ndicho kinanogesha sifa hii

Usipomsifu Mungu sasa ukiwa na afya unategemea nini?



Natamani ungekuwepo na wewe tusifu pamoja.

WRM KUMECHANGAMKA NATAMANI UFIKE UUNGANE NA WAPENDWA HAWA

Mchungaji Anna Nicolaus wa kwanza mbele akimsifu Mungu

Waone hawa wakimtukuza Mungu katika ibada ya leo Jumapili



Asikwambie mtu bwana ona mwenye watu wazima hawa wakimsifu Mungu ndani ya WRM

KARIBU WRM IBADA INAENDELEA SASA MATEMBELE YA PILI KIVULE


Unakaribishwa katika Huduma ya The Word of Recopnciliation Ministries (WRM) iliyo chini ya Nabii Nicolaus iliyopo Matembele ya Pili Kivule jijini Dar es Salaam. Ibada inaendelea sasa, unakaribishwa ibada hii ya kwanza inayoisha saa 7:00 mchana.
Baadhi ya waimbaji wa Sauti za Sifa wa  wakimsifu Mungu hivi sasa katika madhabahu hiyo.


Mpiga gita wa huduma hiyo Emmanuel akiwa kazini

Mpiga tumba wa huduma hiyo Kejo akizichalaza vema ngoma hizo

Baadhi ya waimbaji wa Sauti za Sifa wa  wakimsifu Mungu hivi sasa katika madhabahu hiyo.


Older Posts